• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Dawati la Malalamiko |
KILOSA DISTRICT COUNCIL
KILOSA DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Idara
      • Utumishi
      • Fedha na Biashara
      • Afya
      • Mipango
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maji
      • Usafi na Mazingira
      • Mifungo na Uvuvi
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Ardhi na Maliasili
      • Ujenzi
    • Vitengo
      • sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi
      • TEHAMA
      • Uchaguzi
      • Nyuki
    • Muundo wa Halmashauri
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba Mbalimbali
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Ripoti
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Tangazo
    • Maktaba
    • Hotuba
    • Vyombo vya Habari
    • Video

KILOSA YAASWA KUSHIKILIA REKODI YA KUWA NA HATI INAYORIDHISHA

Posted on: May 7th, 2020

Licha ya kutoa pongezi kwa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Loata Ole Sanare ameitaka Halmashauri kuendelea kulinda mafanikio waliyoyapata ya kupata hati inayoridhisha kwa kuhakikisha inaondoa makando kando yote yanayosababisha kuwa na hati isiyoridhisha ambapo kwa miaka minne mfululizo kuanzia mwaka 2015/16,  2016/17,  2017/18 na 2018/19 Kilosa imekuwa ikipata hati inayoridhisha.


Sanare ametoa rai hiyo Mei 6 mwaka huu wakati wa baraza maalum la madiwani kwa ajili ya kujadili taarifa na majibu ya hoja za mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali za mwaka wa fedha 2018/19 ambapo ametaika Halmashauri kuendelea na mwenendo wa utendaji kazi mzuri kwa kuepuka kufanya kazi kwa mazoea hususani kwa watendaji na wasimamizi wa shughuli za kimaendeleo ndani ya Halmashauri. 

Sanare amesema mkaguzi katika taarifa yake ameonyesha kumekuwa na udhaifu katika baadhi ya maeneo ikiwemo kutozingatiwa kwa baadhi maelekezo ya serikali ambayo yamesababisha hoja ambazo hazijafungwa hivyo ametaka hoja zote ambazo hazijafungwa ziweze kushughulikiwa ipasavyo na hoja zote zinazojitokeza kutekelezwa ipasavyo ili kuepusha uwepo wa hoja huku akilitaka baraza la madiwani kuchukua hatua kwa watumishi wote waliosababisha kuwepo kwa hoja.


Pamoja na hayo amewataka madiwani kuhimiza utekelezaji wa miradi ya maendeleo pamoja na kuhamasisha wananchi kuchangia miradi ya maendeleo na kuhakikisha miradi inayoanzishwa inakamilishwa ikiwemo kuwachukulia hatua watumishi wanaosababisha ubadhilifu wa fedha katika miradi hiyo.

Aidha ametaka kufanyika usimamizi wa kutosha katika utendaji kazi wa serikali ili kudhibiti uwepo wa hoja kwa kuzingatia taratibu, sheria na kanuni za utendaji kazi serikalini,  huku akitaka kuwepo kwa uadilifu katika matumizi ya fedha za Serikali ambapo pia ametaka wakuu wa idara wanaokaimu nafasi za ukuu wa idara kwa muda mrefu kufanyika mchakato wa kuhakikisha nafasi hizo zinakuwa na wakuu wa idara kamili badala ya makaimu hao kukaa katika nafasi hizo kwa muda mrefu.


Akizungumzia upande wa mapato amesema kiasi cha fedha kilichokusanywa ni nusu ya malengo yaliyokusudiwa hivyo ametaka kufanyika kwa tafiti na ufuatiliaji wa makusanyo katika maeneo yote kwani ili shughuli za maendeleo zifanikiwe lazima kuwe na makusanyo ya aina mbalimbali kupitia kodi na tozo mbalimbali.

Akihitimisha maagizo na maelekezo yake Sanare ametaka kuundwa kwa timu maalumu ya kufanya ukaguzi kwa wasambazaji wa sukari na kuhakikisha sukari inakuwepo maeneo yote na inauzwa kwa bei elekezi ya shilingi 2700 kwa kilo kwa kila duka na kwa yoyoyte atakayebainika kuuza sukari kwa bei ya juu hatua stahiki zichukuliwe dhidi yake ikiwemo wale wauzaji wanaoficha sukari na kusababisha uhaba wa sukari.


Akitoa taarifa mkaguzi wa hesabu za Serikali Peter Mwambwanga amesema utaratibu wa ukaguzi wa matumizi ya fedha za Serikali unalenga kuangalia endapo matumizi ya fedha za Serikali kama yamefuata taratibu stahiki ambapo ukaguzi ulifanyika katika mamlaka za serikali 185 zilizokaguliwa  halmashuri  176 zilifanya vizuri huku Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa ni mojawapo ya Halmashauri zilizofanya vizuri na kwamba katika Mkoa wa Morogoro halmashauri zote 9 zimefanya vizuri na kupata hati inayoridhisha.

Mwambwanga amesema kamati ya bunge ya hesabu za Serikali za mitaa ilitoa maagizo manne kwa ajili ya kuiboresha Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa ambapo maagizo matatu yameshatekelezwa huku moja likiwa katika ngazi ya utekelezaji na kwamba ikifanyika tahmini toka mwaka 2015/16 hadi 2018/19 imekuwa ikipata hati inayoridhisha na kwamba katika maoni 37 yaliyotolewa kwa halmashuri maoni 30 yameshafanyiwa kazi kikamifu na kubakiza maoni 7 ambayo ni sawa na asilimia 81 ya utekelezaji.


Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashuri ya Wilaya ya Kilosa Asajile Mwambambale amesema kuwa maagizo na maelekezo yaliyotolewa kama halmashauri wameyachukua na kuyafanyia kazi  huku akimshukuru Mkuu wa Mkoa kwa ziara zake ambazo zimekuwa zikichagiza na kuboresha utendaji kazi na usimamizi ndani ya wilaya lengo likiwa ni utoaji wa huduma kwa jamii ambao ndo msingi ndio dhamira ya Serikali ya awamu ya tano chini Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli.

Mwambambale amesema kama halmashuri wanajitahidi kuzingatia maelekezo ya mkaguzi mkuu wa hesabu za Serikali na ndio maana kumekuwa kunakupungua kwa hoja hizo na anawashukuru waheshimiwa madiwani na watendaji kwa ushirikiano wao na kwamba kama halmashuri wanajipanga kuhakikisha hoja hizo zinapungua zaidi na ikiwezekana halmashuri kutokuwa na hoja kabisa.


Tangazo

  • MAJINA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA KWA MWAKA 2021 December 18, 2020
  • MAELEKEZO YA KUJIUNGA (JOINING INSTRUCTION) KIDATO CHA KWANZA 2021 KATIKA SHULE ZA SEKONDARI ZA HALMASHAURI YA WILAYA KILOSA December 24, 2020
  • ZABUNI January 31, 2017
  • SOMA KATIBA ILIYOPENDEKEZWA March 24, 2017
  • Angalia zote

Habari za sasa

  • WAKUU WA SHULE WATAKIWA KUMALIZA UJENZI WA MADARASA - MGOYI

    January 15, 2021
  • MKANDARASI LUKOLO CONSTRACTOR ATAKIWA KUMALIZA MRADI KWA WAKATI- KUSAYA

    January 15, 2021
  • KILOSA YAJIPANGA KUTOPOTEZA VIPINDI MADARASANI

    January 12, 2021
  • RC MORO AWACHUKULIA HATUA WENYEVITI WA VITONGOJI MIKUMI

    January 07, 2021
  • Angalia zote

Video

HIFADHII YA WANYAMA MIKUMI
Video zaidi

Kurasa za Haraka

  • CHF ILIYOBORESHWA
  • MKATABA WA HUDUMA KWA MTEJA
  • MFUMO WA FFARS
  • MFUMO WA KIBALI KUSAFIRI NJE YA NCHI
  • MFUMO WA PLANREP

Kurasa za Mfanano

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • NECTA
  • Jamhuri ya Muungano Tanzania
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Mkoa Morogoro

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Eneo la Ramani

Wasiliana Nasi

    Halmashauri ya Wilaya Kilosa

    Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa

    Simu: 023 2623093

    Simu: +255714800948

    Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa