• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Dawati la Malalamiko |
KILOSA DISTRICT COUNCIL
KILOSA DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Idara
      • Utumishi
      • Fedha na Biashara
      • Afya
      • Mipango
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maji
      • Usafi na Mazingira
      • Mifungo na Uvuvi
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Ardhi na Maliasili
      • Ujenzi
    • Vitengo
      • sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi
      • TEHAMA
      • Uchaguzi
      • Nyuki
    • Muundo wa Halmashauri
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba Mbalimbali
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Ripoti
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Tangazo
    • Maktaba
    • Hotuba
    • Vyombo vya Habari
    • Video

SIMAMIENI SUALA LA LISHE KATIKA MAENEO YENU

Posted on: December 23rd, 2020

Watendaji wa kata wametakiwa kuhakikisha wanasimamia vyema suala zima la lishe katika maeneo yao ikiwemo kutunga sheria ndogo ndogo zinazoelekeza usimamizi wa makuzi na malezi muhimu kwa watoto lengo ikiwa ni kuhakikisha wilaya inakuwa na kizazi kilicho bora chenye kuzingatia hatua zote muhimu katika ukuaji wa mtoto toka anapokuwa tumboni hadi kuzaliwa sambamba na kuzingatia upatikanaji na matumizi ya lishe bora kwa mama mjamzito hadi mtoto chini ya umri wa miaka mitano.


Agizo hilo limetolewa Disemba 23 mwaka huu na Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Adam Mgoyi wakati wa kikao cha kamati ya lishe na watendaji wa kata ambapo ametaka kila kata na kijiji kuwa na sheria ndogo ndogo ambazo zinapaswa kutekelezwa na jamii husika katika kuhakikisha malezi na makuzi ya mtoto yanazingatiwa ipasavyo kwa kuzingatia uhudhuriaji wa kliniki kwa mama mjamzito na suala zima la lishe ili kuepusha watoto kutokuwa na utapiamlo kwani lishe ndiyo inayojenga msingi wa ukuaji wa mtoto.

Mgoyi amesema endapo mtoto atakosa lishe bora itapelekea kupata utapiamlo lakini pia kuwa na ufaulu wa chini shuleni, hivyo kila mmoja kwa sehemu yake anao wajibu wa kushiriki kikamilifu kwa kushirikiana na wahudumu wa afya waliowezeshwa kutoa elimu ya lishe majumbani ili kuisaidia jamii kuzingatia upatikanaji na matumizi ya lishe bora jambo litakaloleta matokeo chanya kwa jamii huku akitaka suala la lishe kuwa ni ajenda muhimu katika vikao vya mabaraza ya maendeleo ya kata na vijiji ambapo amesisitiza kuwa endapo litazingatiwa itasaidia wilaya kiujumla kuwa na takwimu sahihi za lishe kwa kila kata na kijiji pia kila kijiji kinapaswa kuweka utaratibu wa kuadhimisha siku ya lishe kwa kila kijiji ambapo jamii itapata wasaa wa kupata elimi ya makuzi na malezi ya mtoto pamoja na lishe.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa Asajile Mwambambale amewataka watendaji hao kushirikiana kwa ukaribu na wahudumu wa afya wanaotoa elimu ya lishe majumbani kwa kuhakikisha wanatoa elimu hiyo ikwemo kusimamia matumizi ya baiskeli walizopewa kutotumika kwa matumizi binafsi badala yake zitumike kama ilivyokusudiwa kama chombo cha usafiri ili kuifikia jamii na kutoa elimu na kwamba kupitia ushiriki wao itasaidia kufanya ufuatiliaji jambo litakalosaidia kujua hali ya lishe kiuhalisia katika maeneo yao ya kiutawala.

Akifunga kikao hicho Katibu Tawala Wilaya Yohana Kasitila  amesema suala la lishe ni ajenda muhimu sana kwa watendaji wa kata kushiriki kikamilifu pia amewataka kutatua kero za wananchi kupitia vikao badala ya kusubiri kero hizo kufikishwa kwa Mkuu wa Wilaya au Mkurugenzi wakati kero hizo zinatakiwa zitatuliwe katika ngazi za vijiji na kata lakini pia wametakiwa kujipima utendaji wao wa kazi huku akisisitiza usimamizi wa usomaji wa taarifa za mapato na matumizi, kufanyika kwa vikao vya kisheria, usimamizi wa sheria mbalimbali na utekelezaji wake sambamba na kujiwekea mpango kazi wa majukumu yao.


Tangazo

  • MAJINA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA KWA MWAKA 2021 December 18, 2020
  • MAELEKEZO YA KUJIUNGA (JOINING INSTRUCTION) KIDATO CHA KWANZA 2021 KATIKA SHULE ZA SEKONDARI ZA HALMASHAURI YA WILAYA KILOSA December 24, 2020
  • ZABUNI January 31, 2017
  • SOMA KATIBA ILIYOPENDEKEZWA March 24, 2017
  • Angalia zote

Habari za sasa

  • WAKUU WA SHULE WATAKIWA KUMALIZA UJENZI WA MADARASA - MGOYI

    January 15, 2021
  • MKANDARASI LUKOLO CONSTRACTOR ATAKIWA KUMALIZA MRADI KWA WAKATI- KUSAYA

    January 15, 2021
  • KILOSA YAJIPANGA KUTOPOTEZA VIPINDI MADARASANI

    January 12, 2021
  • RC MORO AWACHUKULIA HATUA WENYEVITI WA VITONGOJI MIKUMI

    January 07, 2021
  • Angalia zote

Video

HIFADHII YA WANYAMA MIKUMI
Video zaidi

Kurasa za Haraka

  • CHF ILIYOBORESHWA
  • MKATABA WA HUDUMA KWA MTEJA
  • MFUMO WA FFARS
  • MFUMO WA KIBALI KUSAFIRI NJE YA NCHI
  • MFUMO WA PLANREP

Kurasa za Mfanano

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • NECTA
  • Jamhuri ya Muungano Tanzania
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Mkoa Morogoro

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Eneo la Ramani

Wasiliana Nasi

    Halmashauri ya Wilaya Kilosa

    Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa

    Simu: 023 2623093

    Simu: +255714800948

    Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa