• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Dawati la Malalamiko |
KILOSA DISTRICT COUNCIL
KILOSA DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Idara
      • Utumishi
      • Fedha na Biashara
      • Afya
      • Mipango
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maji
      • Usafi na Mazingira
      • Mifungo na Uvuvi
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Ardhi na Maliasili
      • Ujenzi
    • Vitengo
      • sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi
      • TEHAMA
      • Uchaguzi
      • Nyuki
    • Muundo wa Halmashauri
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba Mbalimbali
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Ripoti
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Tangazo
    • Maktaba
    • Hotuba
    • Vyombo vya Habari
    • Video

WAJIBIKENI KWA MUJIBU WA MAJUKUMU YENU

Posted on: September 18th, 2018

Maafisa Tarafa, Watendaji wa Kata na Vijiji wilayani Kilosa wametakiwa kutambua vema majukumu yao licha ya uwepo wa ugumu na changamoto mbalimbali zilizopo ambazo haziwaondolei watumishi hao wa umma  kufanya majukumu yao ipasavyo kwani wameaminiwa na serikali kuwepo kwa maeneo ya kazi, hivyo wanapaswa kufanya majukumu yao kwa kuzingatia sheria, taratibu na kanuni za kazi ikiwemo kuwasimamamia kimajukumu watumishi walio chini yao kwa mujibu wa misingi ya utawala bora kwa kuhakikisha wanafanya majukumu yao ipasavyo kwa kuwahudumia wananchi.

Rai hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa Asajile Mwambambale wakati wa kikao cha Mkurugenzi huyo kilichoshirikisha Wakuu wa Idara na Vitengo, Maafisa Tarafa, Watendaji wa Kata na Vijiji ambapo amewataka watumishi hao kusimamia na kukusanya mapato ya Halmashauri  kwa kuzingatia uadilifu katika ukusanyaji mapato kwa kusimamia maadili ya utumishi wa umma pamoja na utoaji takwimu sahihi na taarifa muhimu kwa wakati kwa maslahi ya Halmashauri na Taifa kwa ujumla.

‘‘Aidha niseme kuwa Maafisa Tarafa, Watendaji wa Kata na Vijiji mnao wajibu wa kusimamia miradi ya maendeleo ili ijengwe kwa ubora na ikamilike  kwa wakati ili wananchi wapate  huduma wanazostahili kwani usimamizi wa miradi ni sehemu ya majukumu yenu ikiwemo utoaji wa taarifa za mara kwa mara kwa viongozi wa juu kwa kila kinachoendelea hasa katika miradi jambo litakalosaidia Halmashauri kutokuwa na hoja zinazoashiria ubadhirifu wa fedha na maswali ya sintofahamu pindi ziara mbalimbali za viongozi zinapojitokeza pamoja na utoaji huduma bora kwa wananchi bila ya ubaguzi, upendeleo wala viashiria vya rushwa’’. Ameongeza Mwambambale.

Aidha katika kikao hicho Wakuu wa Idara walitoa mada mbalimbali kwa watendaji hao lengo ikiwa ni kuwakumbusha majukumu yao kama watumishi wa umma ambapo miongoni mwa mada hizo ni Uwajibikaji na usimamizi wa mapato, Kuzingatia Dhana ya Utawala bora katika uwajibikaji kwa wananchi, Udhibiti na utatuzi wa migogoro ndani ya jamii na kwa wananchi, Uanzishwaji, utunzaji na uhuishaji wa daftari la wakulima, Kampeni ya ujenzi wa vyoo bora kwa afya bora katika jamii, Uhifadhi na utunzaji wa mazingira na kuepuka athari za uharibifu wa mazingira.

Mada nyingine ni Usimamizi wa vibali vya ujenzi na kuzuia ujenzi holela, Kuanzisha na kuhuisha Rejista za wakazi kwenye vitongoji, Maelekezo na maagizo ya Serikali na Halmashauri, Jumuiya za watumia maji vijijini pamoja na Sheria ndogo, Mikataba na Mabaraza ya kata ambapo mwanasheria wa Halmashauri amewataka watendaji hao kutambua kuwa jukumu la kuandaa mikataba ni la Ofisi ya sheria hivyo linapaswa kuzingatiwa ili kuepuka athari mbalimbali zinazoweza kujitokeza ikiwemo kukiukwa kwa taratibu na kanuni za mikataba mbalimbali pamoja na kuepuka kesi ambazo zinazoweza kujitokeza dhidi ya Halmashauri.

Katika kuhitimisha kikao hicho Mkurugenzi Mtendaji amewaagiza watendaji wote kuainisha vyanzo vyote vya  mapato katika maeneo yao pamoja na kuainisha uwezo wa kila chanzo sambamba na kufufa akaunti zote za vijiji ili 20% zinazopaswa kurudishwa katika vijiji kwa mujibu wa sheria ziweze kurudishwa kupitia akaunti hizo kwa ajili ya kufanya maendeleo katika vijiji.

Tangazo

  • KUPATA TAARIFA ZA KIUTUMISHI March 22, 2017
  • ZABUNI January 31, 2017
  • SIKU YA USAFI March 23, 2017
  • SOMA KATIBA ILIYOPENDEKEZWA March 24, 2017
  • Angalia zote

Habari za sasa

  • UWAZI NA USHIRIKISHWAJI DHANA MUHIMU

    February 06, 2019
  • SIKU YA SHERIA UTOAJI HAKI KWA WAKATI:WAJIBU WA MAHAKAMA NA WADAU

    February 06, 2019
  • HALMASHAURI YA KILOSA KUKUSANYA MAPATO KUPITIA VYANZO MBALIMBALI

    February 05, 2019
  • TRC KUHAMISHA MAKABURI KUPISHA UJENZI WA RELI KILOSA

    February 01, 2019
  • Angalia zote

Video

HIFADHII YA WANYAMA MIKUMI
Video zaidi

Kurasa za Haraka

  • CHF ILIYOBORESHWA
  • MKATABA WA HUDUMA KWA MTEJA
  • MFUMO WA FFARS
  • MFUMO WA KIBALI KUSAFIRI NJE YA NCHI
  • MFUMO WA PLANREP

Kurasa za Mfanano

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • NECTA
  • Jamhuri ya Muungano Tanzania
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Mkoa Morogoro

World visitors tracker

world map hits counter

Wasiliana Nasi

    Halmashauri ya Wilaya Kilosa

    Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa

    Simu: 023 2623093

    Simu: +255714800948

    Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz

Other Contacts

   

Visitors Counter

writingMasterThesis

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa