• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Dawati la Malalamiko |
KILOSA DISTRICT COUNCIL
KILOSA DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Idara
      • Utumishi
      • Fedha na Biashara
      • Afya
      • Mipango
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maji
      • Usafi na Mazingira
      • Mifungo na Uvuvi
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Ardhi na Maliasili
      • Ujenzi
    • Vitengo
      • sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi
      • TEHAMA
      • Uchaguzi
      • Nyuki
    • Muundo wa Halmashauri
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba Mbalimbali
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Ripoti
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Tangazo
    • Maktaba
    • Hotuba
    • Vyombo vya Habari
    • Video

Walisababisha upotevu wa fedha za saccos ya walimu Kilosa watazitapika

Posted on: February 28th, 2021

Chama cha Ushirika Saccos ya Walimu Wilaya ya Kilosa kimepoteza fedha zaidi ya shilingi bilioni 1.6 baada ya wanachama na wanufaika wengine kukopa na kushindwa kurejesha kwa wakati kutoka mwaka 2007 hadi 2017 ambapo Mrajisi msaidizi wa vyama vya ushirika Mkoa wa Morogoro amemuagiza Mwenyekiti wa Saccos hiyo kuandaa orodha ya majina ya viongozi na watendaji wake ikiwemo namba za simu na mahali wanakopatikana ambapo walikuwepo kipindi hicho kwa kuzingatia muda aliokaa madarakani na kiasi cha fedha kilichopotea ili waweze kuchukuliwa hatua za kisheria.

Akizungumza katika kikao cha bodi ya Saccos ya Walimu Kilosa kilichofanyika mwishoni mwa wiki Mrajisi Kenneth Shemdoe amesema kuwa inawezekana viongozi hao na watendaji wake hawakuchukua hizo fedha lakini kwasababu walikuwa hawafuati taratibu, sheria na masharti ya chama basi watawajibika kwa mujibu wa sheria ya ushirika ,kifungu cha 126 na kwamba watalazimika kulipa faini kiasi cha shilingi milioni 5 ama kifungo kisichopungua miaka miwili au vyote viwili kwa pamoja lakini pia baada ya kutumikia adhabu hizo atalazimika kulipa hasara aliyosababisha katika chama ambapo pia kwa kuwa fedha hizo ni za umma na kwamba si za mtu binafsi hivyo yeyote aliyeshiriki kuchukua hizo fedha atazitapika na kwamba yeye kama kiongozi atahakikisha zinarudi kwa namna yeyote ile na hakuna hata shilingi itakayosalia mikononi mwa mtu.

Aidha katka kikao hicho wajumbe wamekubaliana kwa pamoja kuweka mikakati ya kukiimarisha chama ambapo pia chama hicho inapaswa kutekeleza maazimio mbalimbali ikiwemo kuhakikisha chama kinaandaa orodha ya wastaafu wote na kuanza kuwalipa kadri fedha zitakavyopatikana, kuongeza wanachama wapya, kutoa mikopo ya dharura ya muda mfupi ambayo itazalisha faida itakayosaidia kukiendesha chama, kufanya taratibu za kupata leseni, kuandaa makisio au bajeti kwa mapato na matumizi na kupitisha katika mkutano mkuu miezi miwili kabla ya mwaka wa fedha kuanza, kuhakikisha hesabu za fedha zinafika kwa mkaguzi wa nje ambaye ni mkaguzi wa vyama vya ushirika, kutoa fomu za uchaguzi ambapo uchaguzi unatarajiwa kufanyika kabla ya tarehe 31 April mwaka huu , kuwasilisha rasmi ya hesabu kila mwaka kabla ya tarehe 31 Januari, kuongeza hisa, kufanya mikutano kwa mujibu wa sheria ikiwemo mkutano mkuu wa mwaka na kuhakikisha chama kinaendeshwa kwa mujibu wa sheria za ushirika .

Tangazo

  • MAJINA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA KWA MWAKA 2021 December 18, 2020
  • MAELEKEZO YA KUJIUNGA (JOINING INSTRUCTION) KIDATO CHA KWANZA 2021 KATIKA SHULE ZA SEKONDARI ZA HALMASHAURI YA WILAYA KILOSA December 24, 2020
  • ZABUNI January 31, 2017
  • SOMA KATIBA ILIYOPENDEKEZWA March 24, 2017
  • Angalia zote

Habari za sasa

  • Kikundi cha KIWASAI chafaidika na vifaranga vya samaki 1000

    April 15, 2021
  • Someni taarifa za mapato na matumizi ili shughuli za maendeleo ziende

    March 19, 2021
  • Simamieni ipasavyo matumizi ya rasilimali za Umma

    March 18, 2021
  • Bilioni 1.2 zatengwa kwa ajili ya mradi wa maji

    March 16, 2021
  • Angalia zote

Video

HIFADHII YA WANYAMA MIKUMI
Video zaidi

Kurasa za Haraka

  • CHF ILIYOBORESHWA
  • MKATABA WA HUDUMA KWA MTEJA
  • MFUMO WA FFARS
  • MFUMO WA KIBALI KUSAFIRI NJE YA NCHI
  • MFUMO WA PLANREP

Kurasa za Mfanano

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • NECTA
  • Jamhuri ya Muungano Tanzania
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Mkoa Morogoro

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Eneo la Ramani

Wasiliana Nasi

    Halmashauri ya Wilaya Kilosa

    Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa

    Simu: 023 2623093

    Simu: +255714800948

    Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa