Zaidi ya bilion 1.27 zimetengwa kwa ajili ya miradi ya maji safi na salama ili wananchi waweze kupata huduma ya maji saa 24 kwa mwaka .
Hayo yamesemwa machi 16 2021 na Meneja wakala wa maji na usafi wa mazingira Ruwasa Wilayani kilosa Injinia Josh Hamisi Chum alipokuwa katika kipindi cha mambo mseto kinachorushwa na Radio Jamii Kilosa wakati akizungumzia wiki ya maji ambayo huadhimishwa kuanzia Machi 16 hadi 22 kila mwaka.
Chum amesema kuwa Halmashauri imetenga kiasi cha shilingi bilioni 1,270,000,000 kwa mwaka wa fedha 2021/2022 kwa ajili ya kumalizia miradi iliyopo katika vijiji mbalimbali wilayani humo ikiwa ni pamoja na kuanzisha miradi mipya sehemu ambako bado kuna changamoto ya upatikanaji wa maji na kueleza kuwa kwasasa Ruwasa imefanikiwa kusambaza maji kwa asilimia 73 kwa upande wa vijiji na mijini asilimia 85
Amesema kuwa kuna baadhi ya vijiji vina changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na vyanzo vya maji kukauka kutokana na shughuli za kibinadamu kama vile kilimo na uchimbaji wa madini ambapo tayari wameshaanza kufanya utafiti wa kubaini maeneo katika vijiji ambavyo havina maji safi na salama ili kuanza kuchimba visima virefu vitakavyosambaza maji katika katika maeneo yate.
Chum amefafanua kuwa maadhimisho ya wiki ya maji duniani kwa wilaya ya Kilosa itaadhimishwa kwa kufanya shughuli mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuzindua mradi wa maji Berega, kukagua uchafuzi wa vyanzo vya maji kata ya Ruaha, kukagua miradi ya maji inayoendelea maeneo ya Kitete, Dumila, Mabwegere, kuhamashisha wananchi kutunza mazingira pamoja na kupokea changamoto za upatikanaji wa maji katika kijiji cha Tindiga .
Hata hivyo amesema kuwa kuna baadhi ya vyanzo vya maji vilivyokuwa vinasambaza maji katika mji wa Kilosa vimeharibika kutokana na mafuriko ya mto Mkondoa ambavyo ni Nguzo sita na Mkondoa hali inayopelekea kuwa na changamoto ya kupatikana kwa maji katika baadhi ya maeneo na kusababisha mgawo wa maji na kuongeza kuwa jitihada zinafanyika ili kubaini vyanzo vingine ili kumaliza tatizo hilo la mgao.
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa