Wananchi wilayani Kilosa wamehimizwa kuchangamkia fursa ya kilimo cha pamba kwani kina tija na faida kubwa .
Rai hiyo imetolewa Januari 15 na Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Mh. Alhaji Majid Mwanga wakati wa ziara ya Balozi wa Pamba nchini Agrey Mwanry ambapo walitembelea kata za kwenye Kata ya Magomeni, Mabwerebwere, Rudewa, Kimamba A, Kimamba B na Tindiga kwa lengo la kuhamasishsa wananchi ili walime pamba..
Akiwa katika ziara maalum ya kutembelea maeneo mbalimbali Mwanry amesema lengo la ziara hiyo ni kuhamasisha wananchi ili walime pamba almaqarufu dhahabu nyeupe kwani kwa sasa sokom lipo hivyo wananchi walime pamba bila mashaka ya uwepo wa soko.
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa