• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Dawati la Malalamiko |
KILOSA DISTRICT COUNCIL
KILOSA DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Idara
      • Utumishi
      • Fedha na Biashara
      • Afya
      • Mipango
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maji
      • Usafi na Mazingira
      • Mifungo na Uvuvi
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Ardhi na Maliasili
      • Ujenzi
    • Vitengo
      • sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi
      • TEHAMA
      • Uchaguzi
      • Nyuki
    • Muundo wa Halmashauri
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba Mbalimbali
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Ripoti
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Tangazo
    • Maktaba
    • Hotuba
    • Vyombo vya Habari
    • Video

DC Kilosa awaasa watendaji wa Kata na Vijiji

Posted on: February 10th, 2022

Watendaji wa kata na vijiji wametakiwa kuridhika na kipato wanachokipata kutokana na majukumu yao  badala kujihusisha na ukusanyaji wa kipato kisicho halali kupitia makusanyo ya fedha za Serikali kwani Serikali imewaamini na kuwaweka ili waweze kuwahudumia wananchi katika maeneo yao lakini pia kufanya kazi kwa kuheshimiana na kuzingatia nidhamu ya kiutendaji kazi.

Wito huo umetolewa Februari 09/02/2022 na Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Alhaj Majid Mwanga wakati wa kikao kazi cha Maafisa tarafa, Watendaji wa kata na Vijiji ambapo amewataka kutambua kuwa wao ni watumishi wa umma ambao Serikali imewaamini hivyo wanapaswa kufuata sheria, taratibu na kanuni kadri zinavyowaelekeza katika utendaji wao wa kuwahudumia wananchi.

Mwanga amesema wapo baadhi ya watendaji wanaofanya kazi bila kuzingatia taratibu za kazi ikiwemo kukiuka usimamizi wa mapato kama inavyostahiki  huku akitoa onyo kwa watendaji ambao wamekuwa wakitumia vibaya madaraka yao badala ya kufanya kazi kwa weledi na kuzingatia taaluma yao vizuri.

Aidha ametaka kila mtendaji kuweka malengo ya ukusanyaji mapato kwa kila katika eneo lake kwa kuzingatia vyanzo vyote vya mapato vilivyopo katika maeneo yao huku akisisitiza kufanyika kwa  zoezi la usafi kila mwisho wa mwezi zoezi ambalo linapaswa kufanyika na watu wote ambapo upande wa mapato amewataka kutambua kuwa moja ya vipimo vinavyotazamwa katika utendaji wao ni ukusanyaji wa mapato ambao kwa sasa umekuwa dhaifu jambo linalopelekea Halmashauri kukusanya kiwango kidogo ilihali mapato yapo ya kutosha ila usimamizi umelegalega.

Pamoja na hayo amesisitiza watendaji hao kutambua kuwa mashine za kukusanyia mapato(POS) ni mali isiyohamishika na kwamba fedha yoyote inayokusanywa kutokana  na vyanzo mbalimbali ipelekwe benki mara moja huku akiagiza vizuizi vyote viimarishwe sambamba  na kuweka usimamizi mzuri wa magulio yote lakini pia ametaka watendaji hao kuendelea kusisitiza wananchi kushiriki zoezi la sensa ya watu na makazi ifikapo mwezi Agosti 2022 sambamba na kuhamasisha wananchi waweze kupata chanjo ya Uviko-19.

Kwa upande wake Katibu Tawala Wilaya Yohana Kasitila amewataka watendaji hao kubadilika katika utendaji wa kazi zao hususani katika suala la ukusanyaji mapato kwa kujiepusha namna yoyote ovu na kuepuka rushwa kwani Serikali iko macho hivyo ni vema wakazingatia zaidi sheria, taratibu na kanuni za kazi lakini pia amewakumbusha kuzingatia uandishi wa barua za kiofisi kwa kufuata ngazi za kimadaraka na kimamlaka pamoja na uvaaji unaozingatia maadili kwa watumishi wa umma.


Tangazo

  • TANGAZO NAFASI ZA KAZI October 11, 2021
  • ZABUNI January 31, 2017
  • SOMA KATIBA ILIYOPENDEKEZWA March 24, 2017
  • UTARATIBU WA UHAMISHO KWA WATUMISHI WA UMMA March 24, 2017
  • Angalia zote

Habari za sasa

  • Kilosa kufanya sensa ya mifugo

    December 29, 2022
  • Kilosa kunufaika na mradi wa BOOST

    December 24, 2022
  • Kilosa yaendelea kutambua juhudi za Serikali kwa Watumishi wa Umma na Wananchi-DED Kilosa

    December 19, 2022
  • -Serikali haitosita kulinda Rasilimali watu kwa maslahi ya Maendeleo ya Taifa- Mh. Mhagama

    December 20, 2022
  • Angalia zote

Video

HIFADHII YA WANYAMA MIKUMI
Video zaidi

Kurasa za Haraka

  • CHF ILIYOBORESHWA
  • MKATABA WA HUDUMA KWA MTEJA
  • MFUMO WA FFARS
  • MFUMO WA KIBALI KUSAFIRI NJE YA NCHI
  • MFUMO WA PLANREP

Kurasa za Mfanano

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • NECTA
  • Jamhuri ya Muungano Tanzania
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Mkoa Morogoro

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Eneo la Ramani

Wasiliana Nasi

    Halmashauri ya Wilaya Kilosa

    Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa

    Simu: 023 2623093

    Simu: 0737-847-880

    Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa