Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Mheshimiwa Alhaj Majid Hemed Mwanga ambae sasa ni Mkuu wa Wilaya ya Mlele mkoani Katavi amekabidhi Ofisi Mkuu wa Wilaya kwa Mkuu wa Wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro Mheshimiwa Shaka Hamdu Shaka
Katika makabidhiano hayo yaliyoshuhudiwa na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Kilosa Mwanga amewashukuru watumishi na wananchi wa wilaya ya Kilosa Kwa ushirikiano wote katika uongozi wake na kuwataka kuendelea kutoa ushirikiano kwa Mkuu wa Wilaya Mpya Shaka Hamdu Shaka .
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya Shaka amesema ataendeleza yote yaliyoachwa na mtangulizi wake na kuahidi kuchapa kazi kwa bidii ya kuwatumikia wananchi wa Kilosa kwa kutatua changamoto zao
Ikumbwe kuwa hivi karibu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan alifanya mabadiliko ya Wakuu wa Wilaya ambapo aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Alhaj Majid Mwanga amehamishiwa Wilaya ya Mlele mkoani Katavi nafasi yake kuchukuliwa na Shaka Hamdu Shaka kwa nafasi ya Mkuu wa Wilaya ya Kilosa.
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa