Katika kuendelea Kuunga mkono juhudu za serikali kwenye sekta ya elimu Hifadhi ya Taifa Mikumi imetoa msaada wa Madawati kwenye Shule za msingi saba zinazozunguka Hifadhi hiyo kwenye kata za Mhenda, Ruhembe na Mikumi ambapo madawati hayo yamepokelewa na Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Mhe. Shaka Hamdu Shaka.
Akizungumza wakati wa kupokea madawati hayo, Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Shaka Hamdu Shaka amewashukuru wadau hao kwa mchango wao na kuongeza kuwa serikali inatambua mchango wa wadau mbalimbali katika sekta ya elimu na itaendelea kushirikiana kuinua taaluma
Ameongeza kuwa wilaya ina uhaba wa madawati elfu kumi na sita kwa sasa serikali inaendelea na kutatua changamoto hiyo ambapo tayari madawati elfu nane yamepatikana na Hadi ifikapo disemba mwaka huu changamoto hiyo itamalizika.
Aidha ameongeza kuwa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa bil.1.8 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa , matundu ya vyoo pamoja na madawati yake hivyo fedha hizo zitaelekezwa kukabiliana na changamoto ya uhaba wa madawati.
Akizungunza katika hafla ya kukabidhi Madawati hayo, kaimu Mhifadhi Mkuu Hifadhi ya Taifa Mikumi. Afisa mwandamizi wa Uhifadhi Buka Alfred amesema wametoa madawati 213 yenye Thamani zaidi ya shilingi milioni 18.
Buka anasema Hifadhi hiyo imekua na utaratibu wa kurejesha kwa Wananchi Ili jamiii iwe mabalozi wa masuala ya uhifadhi hasa watoto wadogo.
Ameongeza kuwa kumekua na tabia ya baadhi ya vijiji vinayozunguka Hifadhi kufanya shughuli kinyume na sheria kwenye Hifadhi ikiwemo uwindaji haramu ,ufugaji , kilimo na kuchoma moto jambo ambalo limekuwa changamoto hivyo utolewaji wa madawati hayo ni kuona matunda ya uhifadhi.
Naye Mkuu wa Kitengo Cha ujirani mwema Hifadhi ya Taifa Mikumi Afisa daraja la kwanza Uhifadhi Hamisi Marwa amezitaja shule hizo kuwa ni shule ya Kitete Msindazi, Mikumi, Mikumi Town, Mikumi Mpya, Mhenda, Kielezo na Ruhembe .
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa