Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Mhe. Shaka Hamdu Shaka amehitimisha na kufunga mafunzo ya miezi 4 ya askari 114 mkupuo wa 20 wa jeshi la akiba yaliyofanyika Agosti 15, 2025 katika viwanja vya shule ya Msingi Mvumi.
Akizungumza na wahitimu na wananchi waliojitokeza katika ghafla hiyo Mhe. Shaka amepongeza na kutoa shukrani za dhati kwa JWTZ kupitia makao makuu na kamanda wa jeshi la akiba kwa kuratibu mafunzo hayo kwa weledi na uzalendo wa hali ya juu na kupelekea Wilaya hiyo kuongeza idadi ya askari kila mwaka.
“Mshauri wa jeshi la Akiba nifikishie pongezi zangu huko, tunaelewa kuwa Jeshi la Akiba ni nguzo muhimu katika mfumo wa ulinzi wa taifa letu. Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatambua wajibu wa kila raia kulinda uhuru, umoja na usalama wan chi yetu.” Alisema Mhe. Shaka
Mkuu huyo wa Wilaya amewataka askari hao mafunzo waliyoyapata yasiishie kwenye kuhItimu bali wakayaishi kama sehemu ya maisha yao ya kila siku katika kusaidia jamii na nchi kwa ujumla hasa wakati wa matukio muhimu na ya msingi ambayo ugusa uzalendo wa kila mmoja.
Pia Mhe. Shaka aliwakumbusha vijana kuwa Taifa letu linahitaji wananchi wenye moyo wa kujitoa kama walivyothibitisha wao na kuwa sehemu ya safu ya ulinzi na usalama.
“Morogoro na Wilaya ya Kilosa zina nafasi kubwa katika uchumi wa nchi kutokana na kilimo na rasilimali nyingne ambapo usalama ni nguzo ya maendeleo, nendeni mkawe chachu ya kuhakikisha usalama inakuwa ajenda endelevu kwa nchi yetu”. Alisema Mhe. Shaka
Katika Hafla hiyo Mhe. Shaka amebainisha kuwa jeshi la Akiba ni chelezo laTaifa ambalo lipo kwa ajili ya kuhakikisha Tanzania inabaki salama yenye mshikamano na kuleta maendeleo.
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa