Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Mhe. Shaka Hamdu Shaka amewataka wananchi kuishi kwa amani, upendo na kuheshimiana ili kuepuka migogoro isiyo na tija.
Mhe. Shaka ameeleza hayo Juni 16, 2025 katika mkutano wa hadhara uliofanyika kata ya Kilangali kijiji cha kiduhi ambapo wananchi wa kijiji hicho waliwasilisha kero mbalimbali ikiwemo migogoro ya wakulima na wafugaji.
Akiwa katika mkutano huo Mkuu uyo wa wilaya amewataka wafugaji na wakulima wa kijiji hicho kuacha migogoro isiyokuwa na tija badala yake wajikite kwenye shughuli za uzalishaji mali ili kujiinua kiuchumi.
Sambamba na hayo Mhe. Shaka amesema serikali ya Kilosa imeshafanya maamuzi ya kurudisha kamati za amani zilizokuwepo kipindi cha awali zinazojumuisha wakulima, wafugaji na watu mashuhuli ziendelee kufanya kazi ili zisaidie kupunguza migogoro hiyo na jamii iweze kuishi kwa amani, upendo na ushirikiano.
Aidha Mhe. Shaka amewatoa hofu wananchi hao na kuwaahidi changamoto zote walizowasilisha amezipokea kwa ajili ya kuzifanyia kazi na kuzitafutia ufumbuzi hivyo waendelee na shughuli zao za kila siku kama kawaida.
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa