Wananchi wa vijiji vya Malangali, Tindiga(A naB), Kwa Lukwambe na Ngaite Wilayani Kilosa wametakiwa kuwa wavumilivu wakati Ofisi ya Mkuu wa Wilaya inatatua migogoro ya mipaka ya vijiji vyao ili kumalizia changamoto hiyo kwa amani.
Wito huo umetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Mhe. Shaka Hamdu Shaka wakati alipofanya mkutano wa hadhara wa kusikiliza changamoto ya migogoro ya ardhi katika vijiji hivyo Oktoba 8, 2025.

Mkuu huyo wa Wilaya ameunda kamati yenye jumla ya wajumbe 8 kwa kila Kijiji kwa ajili ya kutatua changamoto ya ardhi kiwemo mipaka ya ardhi kwa kila kijji
Mhe. Shaka amesema kuwa kamati hizo zitafanya kazi kwa muda wa siku saba kuanzia Oktoba 9, 2025 na maamuzi yatatolewa Alhamis wiki ijayo.

"Kuanzia Leo si Ngaite, Kwa Lukwambe, Tindiga (Ana B), Malangali hatutaki kuona Wala kusikia shughuli yoyote kuingia maeneo hayo kwa kwenda kufanya shughuli zozote za kugawa, ama kilimo, ama shughuli zozote mpaka Siku ya Alhamis tutakapomaliza jambo hili" Alisema Mhe. Shaka.
Hata hivyo Mhe. Shaka amewataka wananchi hao kuheshimu maamuzi ambayo yamehafikiwa kwenye mkutano huo.

Kwa upande wake Mkulima, Bi Esta Moris amemshukuru Mkuu wa Wilaya kwa kuweza kuwasikiliza na kutatua migogoro yako kwa njia ya amani.
Vileviel Mwenyekiti wa Chama Cha Wafugaji kata ya Tindiga Filemoni Karao amesema kuwa wameridhia maamuzi ya Mkuu wa Wilaya ya kuunda kamati itayosimamia na kutatua migogoro hiyo ili kutoa majibu sahihi

Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa