• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Dawati la Malalamiko |
KILOSA DISTRICT COUNCIL
KILOSA DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Divisheni
      • Utawala,Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Viwanda,Biashara na Uwekezaji
      • Huduma za Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Mipango na Uratibu
      • Elimu ya Awali na Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Miundombinu ya Mijini na Vijijini
    • Vitengo
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Usimamizi na Ununuzi
      • TEHAMA na Takwimu
      • Fedha na Uhasibu
      • Maliasili na Mazingira
      • Mawasiliano Serikalini
        • Michezo,Utamaduni na Sanaa
      • Michezo,Utamaduni na Sanaa
      • Usimamizi wa Taka Ngumu na Usafi wa Mazingira
    • Muundo wa Halmashauri
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba Mbalimbali
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Ripoti
    • Jarida la Mtandaoni
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Tangazo
    • Maktaba
    • Hotuba
    • Vyombo vya Habari
    • Video

Fanyeni Kazi Kwa Kushirikiana na Kufuata Taratibu- DC Kilosa

Posted on: July 20th, 2021

Rai imetolewa kwa viongozi mbalimbali kufanya kazi kwa ushirikiano na maelewano lengo ikiwa ni kuhakikisha kunakuwa na uongozi wa pamoja wenye kuleta maendeleo ambapo imebainishwa kuwa changamoto nyingi huanzia katika ngazi ya kijiji hivyo ni vema kila mmoja akabadilika katika utendaji wake wa kazi badala ya kutumia madaraka yao kinyume na inavyostahiki ili kutoleta migogoro.

Mkuu wa wilaya ya Kilosa Alhaji Majid Mwanga ametoa rai hiyo Julai 19 mwaka huu wakati wa kikao cha kamati ya uvunaji wa misitu ambapo amesema uongozi wa pamoja ni kitu cha muhimu kwani utendaji wa Serikali unahitaji kila mmoja kumtambua kiongozi mwenzake kama sehemu yake ya kazi kwani kwa kufanya hivyo itasaidia kazi kufanyika katika utaratibu mzuri na ushirikiano huku akisisitiza taratibu za kiutendaji kufuatwa kwa mujibu wa taratibu,sheria na kanuni huku akitaka kufuatwa kwa taratibu za kila sekta kama zinavyoelekeza ikiwemo kutotumika vibaya kwa madaraka waliyonayo ambapo ametaka maafisa tarafa, watendaji wa kata, watendaji wa vijiji na wenyeviti wa vijiji pamoja na wataalam kufanya kazi kwa kuheshimiana jambo litakalosaidia kuwa na timu moja yenye mtazamo chanya wa kuleta maendeleo.

                                                      Afisa Maliasili Mkoa John Chuwa

                                                    Mhifadhi Misitu Mkuu Wilaya Samwel Nyabange

Kwa upande wake Afisa Maliasili Mkoa Joseph Chuwa amewataka viongozi wa vijiji kutojihusisha na uvunaji haramu ambapo pia amesisitiza usimamizi shirikishi na uvunaji endelevu ambapo pia ametaka kuwepo kwa umakini kwa majina yanayopitishwa kwa kuzingatia zaidi taratibu zinavyoelekeza  sambamba na kuweka rekodi na kumbukumbu kwani kumekuwa na hulka ya baadhi ya waombaji kuomba maeneo lakini hawayafanyii kazi jambo linalosababisha upotevu wa mapato huku Mhifadhi Misitu Mkuu Wilaya Samwel Nyabange akibainisha sababu zilizopelekea kutofikia malengo ya makusanyo ya fedha ikiwemo mabadiliko ya bei ya mazao ya misitu mwaka 2020, kuongezeka kwa mahitaji ya mbao pandwa katika soko, miundombinu mibovu ya barabara hasa kipindi cha masika, uwepo wa wimbi la ugonjwa wa COVID 19, uchache wa watumishi na vitendea kazi, uwepo wa njia nyingi za utoroshaji wa mazao ya misitu migogoro ya mipaka kati ya Wilaya na Wilaya, vijiji na vijiji.

Katika kuhakikisha udhibiti wa misitu unafanyika ipasavyo Kamanda wa TAKUKURU Wilaya Gwakisa Mwaikela amesema zipo namna mbalimbali za kufanya udhibiti ili kutopoteza mapato ikiwemo kuhakikisha magogo yote yanayovunwa yanagongwa muhuri eneo husika la kuvunia ikiwemo kudhibiti wavunaji wote wasiovuna maeneo stahiki waliyoomba ama kuvuna kiasi pungufu ya walichoomba sambamba na kuwadhibiti kwa kutowapa leseni ama kibali kwa mara nyingine endapo hawatavuna kwa mujibu wa makubaliano ambapo pia ameshauri kutoruhusiwa kwa mvunaji yoyote pasipokuwa na risiti ya ushuru wa kijiji inayomruhusu kuvuna baada ya kulipia jambo litakalosaidia vijiji na Halmashauri kuingiza mapato.

Akieleza taarifa ya upandaji miti Afisa Maliasili Wilaya John Mtimbanjai amesema  ili kukabiliana na changamoto ya kutoweka kwa rasilimali ya Misitu, jamii inahamasishwa kupanda miti katika maeneo wanayoishi, maeneo ya taasisi na maeneo ya mashamba binafsi ya wananchi huku upande wa mikakati iliyopo kuzuia uharibifu wa misitu hii ni pamoja na kuendelea kutenga bajeti na kushirikiana na wadau kuwezesha Mipango ya Matumizi bora ya ardhi ya vijiji, kuainisha mipaka ya misitu ya hifadhi za serikali kuu, halmashauri na vijiji kwa kuweka beacons/alama na kufyekea barabara ya mipaka inayotenga hifadhi na maeneo ya vijiji, kuelimisha jamii kuhusu umuhimu wa misitu hii kwa ustawi na maendeleo ya jamii, kufanya doria za mara kwa mara ndani na nje ya misitu ili kudhibiti uharibifu, kushirikisha kamati za maliasili za vijiji na jamii kwa ujumla katika kulinda rasilimali za nchi, kuanzisha bustani za miti vijijini ili kupanda miti katika maeneo yaliyoharibiwa na pia kugawa miche kwa wananchi ili wapande katika maeneo yao, kusisitiza kufuata sheria na taratibu za kupata vibali kabla ya kufyeka misitu au kukata miti, kuchukua hatua kwa wanaokiuka taratibu za kuvuna au kukata miti na kufanya ufuatiliali hali ya uvunaji katika vijiji vinavyovuna mazao ya misitu.



Tangazo

  • TANGAZO LA MKUTANO WA BARAZA LA WAHE. MADIWANI May 22, 2025
  • Tangazo la kuanzishwa Dawati Maalum la kushughulikia Migogoro ya Wakulima na Wafugaji November 13, 2024
  • Tangazo la Dawati la Msaada wa Kisheria November 13, 2024
  • TANGAZO LA BARAZA LA MADIWANI LA RISIMU NA MAPENDEKEZO YA MPANGO NA BAJETI KWA MWAKA WA FEDHA 2025/2026 February 25, 2025
  • Angalia zote

Habari za sasa

  • WAUGUZI WATAKIWA KUWA WAADILIFU MAHALI PA KAZI

    May 30, 2025
  • WAHE. MADIWANI WAISHUKURU SERIKALI YA AWAMU YA SITA KWA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO

    May 30, 2025
  • KILOSA YAJIPANGA KUTATUA MIGOGORO YA WAKULIMA NA WAFUGAJI

    May 28, 2025
  • VITENGO VYA HABARI SERIKALINI VIIMARISHWE KWA KUFANYA MAWASILIANO YA KIMKAKATI

    May 24, 2025
  • Angalia zote

Video

RAIS SAMIA ATENGA BILIONI 7.2 KUENDELEZA BONDE LA RUHEMBE
Video zaidi

Kurasa za Haraka

  • e-Mrejesho
  • CHF ILIYOBORESHWA
  • MKATABA WA HUDUMA KWA MTEJA
  • MFUMO WA FFARS
  • MFUMO WA PLANREP
  • MFUMO WA KIBALI KUSAFIRI NJE YA NCHI

Kurasa za Mfanano

  • e-Mrejesho
  • Mkoa Morogoro
  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Jamhuri ya Muungano Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Eneo la Ramani

Wasiliana Nasi

    Halmashauri ya Wilaya Kilosa

    Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa

    Simu: 023 2623093

    Simu: 0737847880

    Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa