• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Dawati la Malalamiko |
KILOSA DISTRICT COUNCIL
KILOSA DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Divisheni
      • Utawala,Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Viwanda,Biashara na Uwekezaji
      • Huduma za Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Mipango na Uratibu
      • Elimu ya Awali na Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Miundombinu ya Mijini na Vijijini
    • Vitengo
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Usimamizi na Ununuzi
      • TEHAMA na Takwimu
      • Fedha na Uhasibu
      • Maliasili na Mazingira
      • Mawasiliano Serikalini
        • Michezo,Utamaduni na Sanaa
      • Michezo,Utamaduni na Sanaa
      • Usimamizi wa Taka Ngumu na Usafi wa Mazingira
    • Muundo wa Halmashauri
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba Mbalimbali
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Ripoti
    • Jarida la Mtandaoni
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Tangazo
    • Maktaba
    • Hotuba
    • Vyombo vya Habari
    • Video

Kambi za kujitambua, kujithamini na kujiamini ziwe endelevu

Posted on: June 22nd, 2021

Rai imetolewa kwa uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa na shule za sekondari kujenga msingi endelevu wa kuwa na kambi za watoto wa kike kipindi cha likizo lengo ikiwa ni kuwaweka pamoja ili waweze kujifunza masomo mbalimbali ikiwemo lugha ya kiingereza na elimu mbalimbali jambo litakalowasaidia kujitambua, kujithamini na kuwa na muda zaidi wa kujenga uelewa wa masomo yao.

Rai hiyo imetolewa na Mkurugenzi Msaidizi Elimu ya Awali na Msingi OR-TAMISEMI Bi. Suzan Nyarubamba wakati wa ufunguzi wa kambi ya mafunzo kwa mtoto wa kike Kilosa iliyoandaliwa na Mbunge wa jimbo la Kilosa ambapo amesema kupitia kambi hizo anaamini zitaleta mabadiliko kwa mtoto wa kike na kumtengenezea mazingira mazuri kielemu na kujitambua huku akiagiza kuanzishwa kwa kambi za jinsia mashuleni zitakazokuwa zikifundisha stadi za maisha, utunzaji wa mazingira, elimu ya ukimwi na masomo mengineyo.

Aidha ametaka kufanyiwa marekebisho kwa sheria kandamizi kwa mtoto wa kike ambazo zinakwamisha kufikiwa kwa ndoto za mtoto wa kike huku akiwataka waheshimiwa madiwani kuhimiza wananchi kuibua watoto wenye mahitaji maalum ili waweze kupata elimu na stahiki zao.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Kilosa ambaye pia ni Waziri wa Sheria na Katiba Prof. Palamagamba Kabudi amesema kambi hiyo inayofanyika shule ya sekondari Dakawa inajumuisha wanafunzi wakike 220 toka shule za sekondari 22 za kata katika jimbo la Kilosa inalenga kuhamasisha wasichana katika shule za sekondari kujitambua, kujithamini na kujiamini pamoja na kuwaunganisha wasichana kuainisha fursa na changamoto zilizopo kijamii, kiuchumi na kitaaluma.

Kabudi amesema kupitia kambi hiyo yenye kauli mbiu ya #Msichana wa Kilosa Timiza Malengo kwa Ustawi wa Kilosa Yetu watajifunza kuhusu stadi za maisha, elimu ya ukimwi, masomo ya sayansi na kiingereza, historia ya nchi pamoja na safari ya mafunzo katika Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine(SUA) huku akisema kambi hizo zinatarajiwa kufanyika kila mwaka  na kwamba kwasasa zimeanza na wasichana ambao kwa asilimia kubwa huathirika na changamoto mbalimbali ikiwemo mimba za utotoni, ndoa za utotoni na changamoto nyinginezo ambapo kwa siku za baadae kambi hizo zitahusisha na wanafunzi wakiume.

Sambamba na hayo amesema Serikali ina mpango wa kuendelea kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa shule za kata na kwamba kupitia mpango wa kuboresha elimu inakusudia kuboresha elimu kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum ikiwemo shule ya msingi Mazinyungu.



Tangazo

  • TANGAZO LA KONGAMANO LA VIJANA WILAYANI KILOSA April 04, 2025
  • Tangazo la kuanzishwa Dawati Maalum la kushughulikia Migogoro ya Wakulima na Wafugaji November 13, 2024
  • Tangazo la Dawati la Msaada wa Kisheria November 13, 2024
  • TANGAZO LA BARAZA LA MADIWANI LA RISIMU NA MAPENDEKEZO YA MPANGO NA BAJETI KWA MWAKA WA FEDHA 2025/2026 February 25, 2025
  • Angalia zote

Habari za sasa

  • VIONGOZI WA VYAMA VYA SIASA WAMETAKIWA KUHAMASISHA WANANCHI KUBORESHA TAARIFA ZAO

    May 07, 2025
  • RC MALIMA AWATAKA WAAJIRI MOROGORO KUTATUA CHANGAMOTO ZA WATUMISHI WAO

    May 01, 2025
  • WALIMU WAPYA 74 WILAYANI KILOSA WAPEWA MAFUNZO ELEKEZI KUHUSU MAADILI NA HAKI ZA UTUMISHI WA UMMA

    April 29, 2025
  • KILOSA YABORESHA USIMAMIZI NA UFATILIAJI WA MIKOPO YA 10% KWA UNUNUZI WA GARI JIPYA

    April 29, 2025
  • Angalia zote

Video

RAIS SAMIA ATENGA BILIONI 7.2 KUENDELEZA BONDE LA RUHEMBE
Video zaidi

Kurasa za Haraka

  • e-Mrejesho
  • CHF ILIYOBORESHWA
  • MKATABA WA HUDUMA KWA MTEJA
  • MFUMO WA FFARS
  • MFUMO WA PLANREP
  • MFUMO WA KIBALI KUSAFIRI NJE YA NCHI

Kurasa za Mfanano

  • e-Mrejesho
  • Mkoa Morogoro
  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Jamhuri ya Muungano Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Eneo la Ramani

Wasiliana Nasi

    Halmashauri ya Wilaya Kilosa

    Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa

    Simu: 023 2623093

    Simu: 0737847880

    Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa