Wakati shule zikifunguliwa kwa ajili ya wanafunzi kuanza rasmi masomo yao Januari 11 mwaka huu mkoa wa Morogoro upande wa elimu sekondari umejipanga kuishi katika kauli mbiu ya hakuna kipindi kupotea lengo likiwa ni kuhakikisha wanafunzi wanafaulu katika kiwango kizuri kinachoridhisha.
Hayo yamebainishwa na Mkuu wa shule ya Sekondari Mazinyungu Ngamba Manegese ambapo amesema licha ya mkoa wa Morogoro kuishi katika kauli hiyo halikadhalika Wilaya ya Kilosa itasimamia kauli hiyo kwa kushirikisha walimu, wazazi na wanafunzi kwani mwanafunzi hawezi kuwa na ufaulu mzuri endapo hatashiriki vizuri katika vipindi hivyo .
Akizungumzia upande wa shule ya Sekondari Mazinyungu amesema wamejipanga kuhakikisha ufaulu wa watoto unakuwa mzuri kwa kuwa na ushirikiano mzuri baina ya wazazi, walimu na wanafunzi pamoja na uwepo wa mitihani ya mara kwa mara huku akimshukuru Mkuu wa Wilaya, Mkurugenzi Mtendaji na uongozi mzima wa Idara ya Elimu Sekondari kwa namna ambavyo wamekuwa wakitoa ushirikiano wa kutosha ili kufikia malengo.
Ngamba amesema kwa upande wa kidato cha nne wamejipanga kuhakikisha mada zote zinakamilika ifikapo mwezi Mei ili kuwa na muda mzuri na wakutosha ili kufanya marudio jambo litakalowasaidia walimu kuwasaidia wanafunzi maeneo yenye changamoto jambo litakalopelekea kuleta matokeo chanya.
Wakiongea kwa niaba ya wanafunzi wenzao wa kidato cha nne Daimon Lameck na Happiness Msafiri wamesema wamejipanga vizuri kuhakikisha kiwango cha taaluma na ufaulu kinakuwa vizuri ikiwemo kuwa na vikundi vya kujisomea, kuweka kambi ya kidato cha nne shuleni hapo ili kuwa na jambo muda mzuri wa kujisomea .
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa