• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Dawati la Malalamiko |
KILOSA DISTRICT COUNCIL
KILOSA DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Idara
      • Utumishi
      • Fedha na Biashara
      • Afya
      • Mipango
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maji
      • Usafi na Mazingira
      • Mifungo na Uvuvi
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Ardhi na Maliasili
      • Ujenzi
    • Vitengo
      • sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi
      • TEHAMA
      • Uchaguzi
      • Nyuki
    • Muundo wa Halmashauri
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba Mbalimbali
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Ripoti
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Tangazo
    • Maktaba
    • Hotuba
    • Vyombo vya Habari
    • Video

Shule ya Msingi Tambykareli yaanza kutumika rasmi

Posted on: March 6th, 2023

Halmashauri ya wilaya ya Kilosa imeendelea kuneema na fedha mbalimbali toka Serikali Kuu katika kuwaletea maendeleo wananchi katika sekta mbalimbali ikiwemo sekta ya elimu, kwa uwepo wa ujenzi wa shule ya msingi Tambukareli katika kata ya Mikumi

Akizungumzia ujenzi wa shule ya hiyo  ambayo imezinduliwa rasmi tarehe 06/03/2023 Mkuu wa Divisheni ya Elimu Msingi na Awali Bi. Zakhia Fandey amesema ujenzi wa shule hiyo umetokana na fedha kutoka Serikali Kuu chini ya mradi wa GPE LANES II kwa shilingi milioni 400, ambapo shule ina vyumba vya madarasa 11.

Fandey amesema shule hiyo itasaidia kwa kiasi kikubwa kuwapunguzia wanafunzi kutembea umbali mrefu, kuinua ari ya wanafunzi kupenda shule kutokana na uwepo wa mazingira bora ya ujifunzaji.

Akizungumzia faida na umuhimu wa uwepo wa shule hiyo Mratibu wa elimu kata ya Mikumi Yusta Ndelwa amesema kupitia uwepo wa shule hiyo umepunguza mrundikano wa idadi kubwa ya wanafunzi madarasani, lakini pia itaongeza usalama wa wanafunzi waliokuwa wakisoma shule za msingi za Mikumi, Mikumi Mpya na Mikumi Town ambapo awali walikuwa wakivuka barabara lakini kwasasa watakuwa salama zaidi.

Aidha amesema wanaishkuru sana Serikali ya awamu ya sita kwa kuitazama Mikumi kwa jicho la tatu, kwani wamefanikiwa kupata madarasa na madawati ya kutosha sambamba na uwepo wa vyoo stahiki ambavyo pia vimezingatia wanafunzi wenye mahitaji maalum.

Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Ibrahim Chembe amesema kupitia fursa hiyo imewajengea wanafunzi na walimu mazingira  na ari nzuri ya ufundishaji na ujifunzaji ambapo imeanza na wanafunzi 432 kuanzia elimu ya awali hadi darasa la sita na kwamba matarajio ni kuwa na wanafunzi 700 kwa shule nzima.

Sambamba na hayo wamemshukuru Mbunge wa jimbo la Mikumi, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri, Mheshimiwa Diwani wa Mikumi ,viongozi wa kata pamoja na wananchi kwa juhudi mbalimbali walizozionyesha kuhakikisha uwepo wa shule hiyo  kwa maslahi ya wanafunzi.


Tangazo

  • TANGAZO NAFASI ZA KAZI October 11, 2021
  • ZABUNI January 31, 2017
  • SOMA KATIBA ILIYOPENDEKEZWA March 24, 2017
  • UTARATIBU WA UHAMISHO KWA WATUMISHI WA UMMA March 24, 2017
  • Angalia zote

Habari za sasa

  • Mfumo wa TAUSI watambulishwa kwa wafanyabiashara

    March 23, 2023
  • Shule ya Msingi Tambukareli yaanza kutumika rasmii

    March 06, 2023
  • Shule ya Msingi Tambykareli yaanza kutumika rasmi

    March 06, 2023
  • DC SHAKA ASISITIZA UONGOZI WA PAMOJA

    March 01, 2023
  • Angalia zote

Video

HIFADHII YA WANYAMA MIKUMI
Video zaidi

Kurasa za Haraka

  • CHF ILIYOBORESHWA
  • MKATABA WA HUDUMA KWA MTEJA
  • MFUMO WA FFARS
  • MFUMO WA KIBALI KUSAFIRI NJE YA NCHI
  • MFUMO WA PLANREP

Kurasa za Mfanano

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • NECTA
  • Jamhuri ya Muungano Tanzania
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Mkoa Morogoro

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Eneo la Ramani

Wasiliana Nasi

    Halmashauri ya Wilaya Kilosa

    Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa

    Simu: 023 2623093

    Simu: 0737-847-880

    Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa