• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Dawati la Malalamiko |
KILOSA DISTRICT COUNCIL
KILOSA DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Divisheni
      • Utawala,Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Viwanda,Biashara na Uwekezaji
      • Huduma za Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Mipango na Uratibu
      • Elimu ya Awali na Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Miundombinu ya Mijini na Vijijini
    • Vitengo
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Usimamizi na Ununuzi
      • TEHAMA na Takwimu
      • Fedha na Uhasibu
      • Maliasili na Mazingira
      • Mawasiliano Serikalini
        • Michezo,Utamaduni na Sanaa
      • Michezo,Utamaduni na Sanaa
      • Usimamizi wa Taka Ngumu na Usafi wa Mazingira
    • Muundo wa Halmashauri
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba Mbalimbali
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Ripoti
    • Jarida la Mtandaoni
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Tangazo
    • Maktaba
    • Hotuba
    • Vyombo vya Habari
    • Video

SIMAMIENI MIRADI KWA KUZINGATIA MATUMIZI YA VIFAA KWA VIWANGO VILIVYOELEKEZWA NA SERIKALI- DED

Posted on: March 29th, 2020

Wito umetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa Asajile Mwambambale kwa wasimamizi mbalimbali wa miradi na kamati za ujenzi katika kata na vijiji kuhakikisha shughuli zote za ujenzi zinazingatia maelekezo ya viwango vya vifaa vilivyoelekezwa na Serikali.


Mwambambale ametoa maelekezo hayo wakati wa ziara yake ya ukaguzi wa miradi akiwa ameambatana na timu ya menejimenti ya Halmashauri ambapo amesema kuwa vifaa hivyo vinapaswa kukidhi mahitaji na viwango vilivyoelekezwa na Serikali ili kupata matokeo mazuri  ya miradi hiyo ili iweze kudumu kwa muda mrefu na kutumika na vizazi vijavyo.


Akiwa ameambatana na timu ya menejimenti katika kituo cha afya Malolo  ameelekeza kuwa wakati wa kiangazi nguvu kazi ya wananchi ianze kuandaa matofari kwa ajili ya wodi tatu kwa maana ya wodi ya wanaume, wanawake na watoto sambamba na jengo la kuhifadhia maiti, huku akisema kuwa ni matumaini yake kuwa kituo cha Malolo kitakapokamilika kitatoa huduma zote za msingi ili kuwaondolea wananchi adha ya kwenda umbali mrefu kupata huduma huku akisema kituo hicho kitahudumia wananchi wengi toka maeneo mbalimbali.

Aidha amesema kuwa anatarajia kuanzia mwezi Julai kituo hicho kitakuwa kimefanya maandalizi  ya kutosha na kwamba ofisi ya Mkurugenzi inategemea kuanza kupokea mahitaji ya uwezeshwaji wa vifaa na ufundi kwa ajili ya wodi hizo na kwamba kama Wilaya ingependa ujenzi katika kituo hicho kukamilika kwa wakati ili huduma zianze kutolewa mara moja kwa wananchi ambapo kituo hicho kinatarajiwa kukamilika mwezi Mei na kwamba kituo cha afya Malolo ni kituo cha mfano kwani kimejengwa na wananchi wenyewe.

Akijibu changamoto zilitolewa za uhaba wa watumishi wa idara ya elimu na kilimo Mkurugenzi amesema litafanyiwa kazi huku akiitaka idara ya Kilimo kufanyia kazi changamoto ya ugonjwa wa zao la vitunguu,  sambamba na hayo ameahidi kuchimbwa kwa kisima kirefu katika kata ya Malolo kazi itakayofanywa na Halmashauri ili kutatua changamoto ya uhaba wa maji ambayo wananchi wamekuwa wakitumia maji ya mtoni ambayo yamekuwa yakisababisha ugonjwa wa kichocho.-

Kwa upande wa kituo cha afya Mikumi ambacho ujenzi wa wodi mbili za wanawake na wanaume unaendelea amesema kwa siku za baadaye kinatarajiwa kiweze kupata hadhi ya kuwa  sawa na hospitali ili kiweze kuhudmuia wanacnhi wengi kwa kadri inavyowezekana kwani huduma za mahali hapo zinalenga zaidi kuhudumia wananchi kwa bei nafuu lakini pia ametaka ujenzi wa wodi hizo kasi iongezwe ili ifikapo mwezi Aprili wodi hizo ziwe zimekamilika ambapo ujenzi huo unafadhiliwa na fedha za Serikali una unatarajiwa kutumia shilingi milioni 140 na kwasasa uko katika hatua za upauaji.

Nao wananchi wa kata za Malolo na Mikumi wameshukuru kwa ujenzi unaondelea katika maeneo yao kwani kabla ya kuwepo kwa vituo hivyo walikuwa katika adha kubwa ya kutafuta huduma katika maeneo ya jirani ambapo walikuwa wakitumia gharama kubwa ili kupata huduma lakini pia kutembea umbali mrefu jambo linalowagharimu fedha na muda lakini kwa sasa wanashukuru kwani adha hizo zimeanza kutoweka na kwamba wanatarajia huduma zote za msingi zitakapotolewa katika vituo hivyo zitakuwa zimewapunguzia gharama mbalimbali kama za matibabu na usafiri

Tangazo

  • TANGAZO LA KONGAMANO LA VIJANA WILAYANI KILOSA April 04, 2025
  • Tangazo la kuanzishwa Dawati Maalum la kushughulikia Migogoro ya Wakulima na Wafugaji November 13, 2024
  • Tangazo la Dawati la Msaada wa Kisheria November 13, 2024
  • TANGAZO LA BARAZA LA MADIWANI LA RISIMU NA MAPENDEKEZO YA MPANGO NA BAJETI KWA MWAKA WA FEDHA 2025/2026 February 25, 2025
  • Angalia zote

Habari za sasa

  • VIONGOZI WA VYAMA VYA SIASA WAMETAKIWA KUHAMASISHA WANANCHI KUBORESHA TAARIFA ZAO

    May 07, 2025
  • RC MALIMA AWATAKA WAAJIRI MOROGORO KUTATUA CHANGAMOTO ZA WATUMISHI WAO

    May 01, 2025
  • WALIMU WAPYA 74 WILAYANI KILOSA WAPEWA MAFUNZO ELEKEZI KUHUSU MAADILI NA HAKI ZA UTUMISHI WA UMMA

    April 29, 2025
  • KILOSA YABORESHA USIMAMIZI NA UFATILIAJI WA MIKOPO YA 10% KWA UNUNUZI WA GARI JIPYA

    April 29, 2025
  • Angalia zote

Video

RAIS SAMIA ATENGA BILIONI 7.2 KUENDELEZA BONDE LA RUHEMBE
Video zaidi

Kurasa za Haraka

  • e-Mrejesho
  • CHF ILIYOBORESHWA
  • MKATABA WA HUDUMA KWA MTEJA
  • MFUMO WA FFARS
  • MFUMO WA PLANREP
  • MFUMO WA KIBALI KUSAFIRI NJE YA NCHI

Kurasa za Mfanano

  • e-Mrejesho
  • Mkoa Morogoro
  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Jamhuri ya Muungano Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Eneo la Ramani

Wasiliana Nasi

    Halmashauri ya Wilaya Kilosa

    Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa

    Simu: 023 2623093

    Simu: 0737847880

    Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa