Shirika laUmeme Tanzania (TANESCO) wilayani Kilosa limejipanga kikamilifu kumaliza tatizo la kukatika kwa umeme mara kwa mara katika baadhi ya maeneo kunakosababishwa na nguzo chakavu zilizooza ama kuanguka ikiwemo kuwepo kwa miundombinu ya umeme mibovu katika baadhi ya maeneo hususani mtaa wa Mtendeni katika kata yaMkwatani.
Meneja wa Tanesco Wilaya ya Kilosa Daniel Makala Kingu
akiwa katika mahojiano maalumu na Radio Jamii Kilosa
Hayo yamebainishwa na Meneja wa Tanesco Wilaya Kilosa Daniel Makala Kingu ambapo amesema Tanesco Kilosa limejipanga kuondoa nguzo zote zilizooza katika maeneo ya miji na vijijini kwenye laini zinazosafirisha umeme kwenda majumbani na kwamba taratibu za kupata nguzo mpya zimeshafanyika..
Hata hivyo amewaomba wananchi kutoa taarifa mapema Tanesco pindi wanapoona hitilafu ya umeme imetokea katika maeneo yao ili hatua za haraka zichukuliwe kabla madhara makubwa kutokea huku akitoa rai kwa wananchi kuwa na vifaa vya kuzuia umeme ili usilete hitilafu katika majengo ikiwemo waya wa Ethi wa kuzuia radi pindi unapokatika na kurudi usilete madhara ndani ya nyumba.
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa