Timu ya Menejimenti ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa (CMT) ikiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji Bi. Beatrice C. Mwinuka ilifanya ziara ya kutembelea na kukagua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo iliyolenga kuhakikisha miradi inatekelezwa kwa wakati na kwa ubora unaotakiwa.
Katika ziara hiyo iliyofanyika Juni 12, 2025 walitembelea miradi ikiwemo Stendi ya Mabasi Dumila ambapo Bi. Beatrice ameeleza kuwa kupitia mapato ya ndani kiasi cha shilingi Milioni 376.1 kimetegwa kwa ajili ya stendi hiyo.
“ Mradi huo ukikamilika utarahisisha shughuli za usafiri, usafirishaji na ukusanyaji wa mapato lakini pia kutoa huduma bora kwa wananchi”. Alisema Bi. Beatrice
Pia Mkurugenzi huyo amewata waatalamu kushirikiana na wakandarasi kwa kila hatua ya ujenzi ili kurekebisha mapungufu yanayojitokeza ikiwa lengo ni kukamilisha miradi kwa wakati na kwa viwango vyenye ubora unaohitajika kwa kufuata Misingi, kanuni na miongozo iliyopo.
“Turekebishe mapungufu yanayojitokeza na tukatekeleze yale yote tuliyokubaliana ili miradi iweze kukamilika kwa wakati na ubora unaotakiwa.” Alisisitiza
Aidha Wajumbe wa CMT waliwasisitiza wasimamizi wa miradi hiyo umuhimu wa utunzaji wa nyaraka za miradi kuanzia hatua ya mwanzo hadi hatua ya mwisho ya ujenzi.
Miradi mingine iliyotembelewa ni pamoja na jengo la utawala, Ukumbi wa Halmashauri, Nyumba ya Mkuu wa Idara, Zahanati ya Mfulu, Shule ya Msingi Matongola na Stendi ya Malori Dumila.
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa