Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Adam Mgoyi amewataka wananchi na wakulima wa wilayani Kilosa kutumia vyema fursa ya uwepo wa mpango mkakati wa kilimo pamoja na uzinduzi wa msimu wa kilimo kujionea teknolojia mbalimbali ambazo ni mpya na kuweka nia ya dhati ya kuzifanyia kazi teknolojia hizo kwani kupitia kilimo wanayo nafasi ya kujiongezea kipato endapo watalima kwa tija na kuzingatia kanuni bora za kilimo pamoja na matumizi ya mbegu bora.
Hayo yameelezwa na Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Adam Mgoyi wakati akikamkaribisha mgeni rasmi naibu waziri wa kilimo Omary Mgumba wakati wa uzinduzi wa msimu wa kiimo 2017/2018 ambapo amesema kuwa wilaya yankilosa imejiwekea mpango mkakati huo kwa kuhakikisha wakullima wanatumia nguzu zao na kuwasidia kitaalam kwa kuhakikisha wanautambua mpango huo kama nyenzo ya kuwasaidia kujitambua nafasi yao na kutumia mpango huo kujikwaamua kimasha kupitia kilimo.
Mgoyi amesema kuwa mpango huo ulianzan kutumika rasmi mwaka 2017 ambapo matokeo yalikuwa mazuri ambapo hadi sasa uzalishaji umepanda kawa asilimiaa 40 ambapo wataalam wamekuwa na mchango mkubwa kwa kushirikiana na taasisi mbalimbali kusaidia wakulima na juhudi hizo zimekuwa msaada kwa kuwajengea uwezo wakulima hao, sambamba na hayo Mgoyi amesema kuwa kupitia uzinduzi wa msimu huo umewapa wakulima nafasi ya kujionea teknolojia mbalimbali, upatikanaji wa mbegu bora na mambo mengine muhimu yanayowasaidia wakulima kulima kwa tija na kujikomboa dhidi ya umasikini.
Aidha Mgoyi alitumia fursa hiyo kuwasilisha changamoto za wakulima kwa Naibu Waziri Kilimo ikiwemo changamoto ya uwepo wa wakala wa pamba aliyesababisha wakulima kutovuna pamba kama walivyotarajia kutokana na kuletewa madawa yasiyofaa hivyo kupelekea hasara kwa wakulima jambo lililosababisha mkuu wa wilaya huyo kwa mamlaka yake kutamka wazi kuwa wakala huyo hahitajiki tena wilayani Kilosa na hana sifa za kufanya kazi wilayani hapa kutokana na hasara aliyoisababisha kwa wakulima ikiwemo kukataliwa kwa baadhi ya pamba kutokana na kukosa ubora.
Akijibu changamoto hizo Naibu Waziri wa Kilimo Mgumba ameiagiza bodi ya pamba Tanzania kuhakikisha inanunua pamba yote iliyokataliwa wilayani Kilosa na kwamba uongozi wa Halmashauri uhakikishe unafanya sensa kwa wakulima wa pamba kujua kiasi cha pamba kilichokataliwa ili taratibu za manunuzi ziweze kufanyika na mzabuni huyo anayelalamikiwa kuwasababishia wakulima wa pamba hasara haruhusiwi tena kufanya kazi katika wilaya ya Kilosa, aidha ametaka mashamba pori yote yaliyofutwa na Mheshimiwa Rais wa awamu ya tano Mhe. John Pombe Magufuli yagawanywe kwa wananchi kama ilivyokusudiwa na amebainisha kuwa serikali ya awamu ya awamu ya tano inatarajia kuwapatia wakulima wa kilosa matrekta 24 kwa njia ya mkopo ambapo baada ya kulipia matrekta hayo yatakabidhiwa rasmi kwa wakulima ili wayamiliki kikamilifu .
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa