• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Dawati la Malalamiko |
KILOSA DISTRICT COUNCIL
KILOSA DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Idara
      • Utumishi
      • Fedha na Biashara
      • Afya
      • Mipango
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maji
      • Usafi na Mazingira
      • Mifungo na Uvuvi
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Ardhi na Maliasili
      • Ujenzi
    • Vitengo
      • sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi
      • TEHAMA
      • Uchaguzi
      • Nyuki
    • Muundo wa Halmashauri
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba Mbalimbali
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Ripoti
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Tangazo
    • Maktaba
    • Hotuba
    • Vyombo vya Habari
    • Video

Wafanyabiashara waridhia tozo ya shilingi 50,000

Posted on: February 13th, 2021

Wafanyabiashara waliopanga katika vibanda vinavyomilikiwa na Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa vilivyoko katika kata ya Kasiki maeneo ya uhindini wamekubali kulipa tozo ya shilingi 50,000 kwa mwezi kwa kibanda hadi hapo vitakapofanyika vikao vya kisheria mara baada ya mwaka wa fedha 2020/2021 kuisha.

Makubaliano hayo yamefanyika Februari 13 mwaka huu katika kikao cha pamoja baina ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa Asajile Mwambambale na wafanyabiashara hao ambapo ametolea ufafanuzi wa kina tozo halali kwa kibanda kwa mwezi ni 50,000, ambayo ilipitishwa kihalali katika vikao vya kisheria na kwamba tozo hiyo itadumu hadi mwaka wa fedha 2020/2021 utapoisha ambapo pia vikao hivyo vina mamalaka ya kushusha ama kupandisha tozo hiyo kwa kadri itakavyoamua na kuridhiwa na baraza la madiwani.

Itakumbukwa siku chache zilizopita wafanyabiashara hao waliopanga katika vibanda hivyo walifunga vibanda zaidi ya 200 wakiishinikiza Halmashauri kutoza shilingi 30,000 kwa kibanda kwa mwezi huku wakidai baraza la madiwani la Februari 6 mwaka 2020 lilipitisha tozo hizo.

Mwambambale amesema tozo ya shilingi 30,000 ni hoja iliyoibuka katika kikao cha kawaida cha baraza  la kawaida la madiwani Februari 6 mwaka 2020 ambapo kwa mujibu wa sheria  na kanuni  haiwezi kuingia katika utekelezaji kwa kuwa haikufuata kanuni, taratibu na sheria ili kupata nguvu kuingia katika utekelezaji.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa Jumuiya ya wafanyabiashara Kilosa Joshua Charuza amesema wameridhia tozo ya shilingi 50,000 kwa kibanda kwa mwezi mpaka mabadiliko yatakapofanyika kwa kufuata utaratibu  wa kisheria huku akitoa wito kwa wafanyabiashara kulipa kodi hiyo na nyingine ili kuleta maendeleo katika Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa.

Naye mfanyabiashara Fadhili Kondo amelaani vikali upotoshwaji uliofanywa na baadhi ya madiwani kwa wafanyabiashara wa kuwaaminisha kuwa tozo mya 30,000 ni halali huku wakijua kuwa tozo hiyo haipo kisheria na hakuna mahali popote ilipopitishwa hivyo waache kuwachonganisha wafanyabiashara na viongozi wa Halmashauri kwani wanampa wakati mgumu Mkurugenzi kutimiza majukumu yake katika kuiletea maendeleo Kilosa.

Tangazo

  • TANGAZO NAFASI ZA KAZI October 11, 2021
  • ZABUNI January 31, 2017
  • SOMA KATIBA ILIYOPENDEKEZWA March 24, 2017
  • UTARATIBU WA UHAMISHO KWA WATUMISHI WA UMMA March 24, 2017
  • Angalia zote

Habari za sasa

  • Kilosa kufanya sensa ya mifugo

    December 29, 2022
  • Kilosa kunufaika na mradi wa BOOST

    December 24, 2022
  • Kilosa yaendelea kutambua juhudi za Serikali kwa Watumishi wa Umma na Wananchi-DED Kilosa

    December 19, 2022
  • -Serikali haitosita kulinda Rasilimali watu kwa maslahi ya Maendeleo ya Taifa- Mh. Mhagama

    December 20, 2022
  • Angalia zote

Video

HIFADHII YA WANYAMA MIKUMI
Video zaidi

Kurasa za Haraka

  • CHF ILIYOBORESHWA
  • MKATABA WA HUDUMA KWA MTEJA
  • MFUMO WA FFARS
  • MFUMO WA KIBALI KUSAFIRI NJE YA NCHI
  • MFUMO WA PLANREP

Kurasa za Mfanano

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • NECTA
  • Jamhuri ya Muungano Tanzania
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Mkoa Morogoro

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Eneo la Ramani

Wasiliana Nasi

    Halmashauri ya Wilaya Kilosa

    Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa

    Simu: 023 2623093

    Simu: 0737-847-880

    Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa