Wahe. Madiwani Wameishukuru Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Dkt.Samia Suluhu Hassani Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuleta fedha nyingi kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika Halmashauri ya wilaya ya Kilosa.
Hayo yamezungumzwa na Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa Mhe. Hassan Mkopi wakati wa Mkutano wa Baraza la wahe. Madiwani kwa kipindi cha robo ya Tatu kwa mwaka wa fedha 2024/2025 ambalo pia ni baraza la mwisho lililofanyika Mei 30, 2025 katika ukumbi wa FDC- Ilonga huku akisifu usimamizi mzuri wa Timu ya menejimenti.
Mhe. Mkopi ameongeza kuwa katika awamu ya sita Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa imepokea fedha nyingi kutoka serikali kuu kwa ajili ya utekelezaji wa Miradi mbalimbali ya maendeleo hususani katika sekta ya Afya na Elimu.
Kwa upande mwingine akijibu swali lililouzwa na Mhe. Livinus Mhawila Diwani wa kata ya Mikumi kuwa ni mikakati gani inafanyika katika kutatua changamoto ya uvamizi wa tembo mashambani, Mhe. Mkopi amesema Halmashauri hiyo imejipanga madhubuti katika kutatua changamoto ya uvamizi wa tembo katika makazi na mashamba ya wananchi katika kata za Mikumi, Mhenda, Kidodi, Kilangali na Kimamba na kuhatarisha usalama wao ambapo mpaka sasa juhudi za kununua risasi kwa ajili ya kuwaondoa wanyama pori hao zinafanyika kwa kushirikiana na Taasisi ya TANAPA pamoja na TAWA.
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa