• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Dawati la Malalamiko |
KILOSA DISTRICT COUNCIL
KILOSA DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Divisheni
      • Utawala,Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Viwanda,Biashara na Uwekezaji
      • Huduma za Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Mipango na Uratibu
      • Elimu ya Awali na Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Miundombinu ya Mijini na Vijijini
    • Vitengo
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Usimamizi na Ununuzi
      • TEHAMA na Takwimu
      • Fedha na Uhasibu
      • Maliasili na Mazingira
      • Mawasiliano Serikalini
        • Michezo,Utamaduni na Sanaa
      • Michezo,Utamaduni na Sanaa
      • Usimamizi wa Taka Ngumu na Usafi wa Mazingira
    • Muundo wa Halmashauri
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba Mbalimbali
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Ripoti
    • Jarida la Mtandaoni
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Tangazo
    • Maktaba
    • Hotuba
    • Vyombo vya Habari
    • Video

Wakazi wa kijiji cha Chabima mbioni kupata huduma za afya katika zahanati ya Chabima

Posted on: February 4th, 2022

Wakazi wa Kijiji cha Chabima kilichopo kata ya Masanze wilayani Kilosa wamekuwa wakitembea umbali wa kilomita 35  tangu kuanzishwa kwa kijiji hicho ili kuweza kufika hospitali ya wilaya ya Kilosa ili kuweza kupata huduma za kiafya.

Hayo yamebainishwa Februari 3 mwaka huu kijiji hapo wakati Kamati ya CCM ilipotembelea Mradi wa Mkaa endelevu na ujenzi wa zahanati ya kijiji cha Chabima ambapo imebainishwa kuwa wakazoi wa kijiji hicho htembea umbali mrefu ili kupata huduma za kiafya jambo lililopel;ekea kijiji hicho kuadhimia kujenga zahanati ili iweze kuwasaidia kupunguza adha yakutopatikana kwa ukaribu kwa huduma hizo.

Akisoma taarifa hiyo mjumbe wa kamati ya maliasili ya kijiji cha chabima idd Tangula amesema kuwa kijiji hicho kimeanzishwa mwaka 1973 na hakukuwa na zahanati kwa kipindi chote hadi mwaka 2012 ndio ulianza ujenzi wa zahanati inayogharimu milioni 120 ambayo imekamilika kwa nguvu kazi za wananchi,halmashauri ikiwa imetoa milioni 32 na Mweneyekiti wa CCM Wilaya Mh. Ameir Mubarak akitoa mifuko ya saruji 50 na kwamba kwasasa wanamalizia ujenzi wa choo.

Aidha amesema kuwa licha ya kukamilika kwa ujenzi huo bado wanakabiliwa na changamoto ya samani za ofisi, vifaa tiba, bomba la maji na mganga hivyo wameiomba Serikali kuwasaidia ili waweze kuepukana na adha hiyo ambayo inagharimu maisha ya watu hususan wajawazito na watoto chini ya miaka mitano.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kilosa ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya Alhaj Majid Mwanga ameonyesha kutoridhishwa na gharama za ujenzi ambazo hazilingani na ubora wa jengo uliopo ambapo imetumika zaidi ya milioni 86 mpaka sasa.

Mwanga licha ya kasoro zilizopo katika ujenzi huo unaendelea ameitaka Serikali ya kijiji kuhakikisha ujenzi huo unakamilika mara moja na fedha ambayo ipo itumike katika ununuzi wa vitanda vya kujifungulia wazazi ili wananchi waanze kupatiwa matibabu kijijini hapo huku akiahidi kushirikiana na Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji kuhakikisha daktari anapatikana ujenzi utakapokamilika ambapo pia amewahamasisha wananchi hao kuchukua tahadhari dhidi ya uviko-19 kwa kupata chanjo ya Uviko 19.

Tangazo

  • TANGAZO LA KONGAMANO LA VIJANA WILAYANI KILOSA April 04, 2025
  • Tangazo la kuanzishwa Dawati Maalum la kushughulikia Migogoro ya Wakulima na Wafugaji November 13, 2024
  • Tangazo la Dawati la Msaada wa Kisheria November 13, 2024
  • TANGAZO LA BARAZA LA MADIWANI LA RISIMU NA MAPENDEKEZO YA MPANGO NA BAJETI KWA MWAKA WA FEDHA 2025/2026 February 25, 2025
  • Angalia zote

Habari za sasa

  • VIONGOZI WA VYAMA VYA SIASA WAMETAKIWA KUHAMASISHA WANANCHI KUBORESHA TAARIFA ZAO

    May 07, 2025
  • RC MALIMA AWATAKA WAAJIRI MOROGORO KUTATUA CHANGAMOTO ZA WATUMISHI WAO

    May 01, 2025
  • WALIMU WAPYA 74 WILAYANI KILOSA WAPEWA MAFUNZO ELEKEZI KUHUSU MAADILI NA HAKI ZA UTUMISHI WA UMMA

    April 29, 2025
  • KILOSA YABORESHA USIMAMIZI NA UFATILIAJI WA MIKOPO YA 10% KWA UNUNUZI WA GARI JIPYA

    April 29, 2025
  • Angalia zote

Video

RAIS SAMIA ATENGA BILIONI 7.2 KUENDELEZA BONDE LA RUHEMBE
Video zaidi

Kurasa za Haraka

  • e-Mrejesho
  • CHF ILIYOBORESHWA
  • MKATABA WA HUDUMA KWA MTEJA
  • MFUMO WA FFARS
  • MFUMO WA PLANREP
  • MFUMO WA KIBALI KUSAFIRI NJE YA NCHI

Kurasa za Mfanano

  • e-Mrejesho
  • Mkoa Morogoro
  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Jamhuri ya Muungano Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Eneo la Ramani

Wasiliana Nasi

    Halmashauri ya Wilaya Kilosa

    Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa

    Simu: 023 2623093

    Simu: 0737847880

    Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa