• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Dawati la Malalamiko |
KILOSA DISTRICT COUNCIL
KILOSA DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Divisheni
      • Utawala,Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Viwanda,Biashara na Uwekezaji
      • Huduma za Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Mipango na Uratibu
      • Elimu ya Awali na Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Miundombinu ya Mijini na Vijijini
    • Vitengo
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Usimamizi na Ununuzi
      • TEHAMA na Takwimu
      • Fedha na Uhasibu
      • Maliasili na Mazingira
      • Mawasiliano Serikalini
        • Michezo,Utamaduni na Sanaa
      • Michezo,Utamaduni na Sanaa
      • Usimamizi wa Taka Ngumu na Usafi wa Mazingira
    • Muundo wa Halmashauri
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba Mbalimbali
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Ripoti
    • Jarida la Mtandaoni
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Tangazo
    • Maktaba
    • Hotuba
    • Vyombo vya Habari
    • Video

Wananchi wahamasishwa kutunza misitu ya vijiji

Posted on: February 4th, 2022

Kwa kutambua umuhimu na chachu yenye ushawishi katika kusukuma gurudumu la maendeleo katika Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa Kamati ya Siasa Wilaya ikiwa imeambatana na Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya kupitia mradi wa mkaa endelevu imejionea utekelezaji wa utunzaji wa misitu na uvunaji wa mkaa kwenye moja ya vijiji ishirini vinavyoshiriki katika mradi huo katika kijiji cha Chabima kilichopo katika kata ya Masanze.

Akizungumza Februari 3 mwaka huu mbele ya kamati ya hizo Meneja wa Mradi wa Kuleta Mageuzi Katika Sekta ya Mkaa Tanzania (TTCS) Charles Leonard amesema kuwa uanzishwaji wa misitu ya ardhi za vijiji umeweza kusaidia uvunaji endelevu wa rasilimali ambapo mradi huo kwa awamu ya tatu ambao unafanywa na Shirika la kuhifadhi Misitu ya Asili (TFCG) chini ya mradi wa mkaa endelevu unaofadhiliwa na Shirika la Uswisi (SDC) ulianza Disemba 2021 na unatarajiwa kuisha Novemba, 2022 ukiwa na tija ya kuwanufaisha wanakijiji na kuweka mfumo utakaochangiwa na vijiji kwa asilimia saba ambazo zitatumika kutoa mafunzo kwa wanakijiji, kuwasaidia soko na kuhimiza uwekezaji kwenye maeneo yao ambapo amesema vijiji vyenye misitu ya vijiji inatambuliwa kimataifa na imesajiliwa katika  kanzi data ya kidunia ambayo itafaidika kwa kuwezeshwa uhifadhi na usimamizi endelevu wa rasilimali za misitu na kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi sambamba na maendeleo ya wananchi.

Wakizungumza baadhi ya wanakijiji ambao wamenufaika na Mradi huo Beritha Magaga na Hamis Kimota wamesema kabla ya mradi walikuwa wakijishughulisha na kilimo pamoja na ufugaji ila baada ya kupatiwa mafunzo na Mradi wa Mkaa Endelevu walihamasika kujiunga kwenye chama cha uvunaji mkaa ambapo kupitia kipato kitokanancho na mkaa wamefanikiwa katika mambo mbalimbali ikiwamo kujenga nyumba, kujikimu katika mahitaji ya kifamilia, kuanzisha biashara ndogondogo na kujiunga katika vyama vya kuweka na kukopa.

Kwa upande wake Katibu wa CCM Wilaya Shaban  Shemdoe ameushukuru uongozi mzima unaoendesha mradi huo kwa elimu waliyowapatia na kujionea shughuli za utunzaji wa misitu na uvunaji mkaa unavyofanyika na kuwapongeza wanakijiji wa Chabima kwa utunzaji wa Misitu ya asili ambapo pia amewaomba TFCG kushirikiana na wananchi kuongeza upandaji wa miti ili kufidia iliyovunwa na huku akiwasisitiza madiwani kuendelea kutoa elimu ya utunzaji misitu kwa wananchi ambayo itawasaidia kuwa wasimamizi wazuri katika maeneo yao.

Aidha ametoa rai kwa watendaji wa vijiji kufanya kazi kwa ukaribu na wenyeviti wa vijiji hususani katika shughuli za maendeleo zinazofanyika katika maeneo yao ikiwemo kuwaunga mkono katika miradi wanayoanzisha kwa manufaa ya wananchi

Tangazo

  • TANGAZO LA KONGAMANO LA VIJANA WILAYANI KILOSA April 04, 2025
  • Tangazo la kuanzishwa Dawati Maalum la kushughulikia Migogoro ya Wakulima na Wafugaji November 13, 2024
  • Tangazo la Dawati la Msaada wa Kisheria November 13, 2024
  • TANGAZO LA BARAZA LA MADIWANI LA RISIMU NA MAPENDEKEZO YA MPANGO NA BAJETI KWA MWAKA WA FEDHA 2025/2026 February 25, 2025
  • Angalia zote

Habari za sasa

  • VIONGOZI WA VYAMA VYA SIASA WAMETAKIWA KUHAMASISHA WANANCHI KUBORESHA TAARIFA ZAO

    May 07, 2025
  • RC MALIMA AWATAKA WAAJIRI MOROGORO KUTATUA CHANGAMOTO ZA WATUMISHI WAO

    May 01, 2025
  • WALIMU WAPYA 74 WILAYANI KILOSA WAPEWA MAFUNZO ELEKEZI KUHUSU MAADILI NA HAKI ZA UTUMISHI WA UMMA

    April 29, 2025
  • KILOSA YABORESHA USIMAMIZI NA UFATILIAJI WA MIKOPO YA 10% KWA UNUNUZI WA GARI JIPYA

    April 29, 2025
  • Angalia zote

Video

RAIS SAMIA ATENGA BILIONI 7.2 KUENDELEZA BONDE LA RUHEMBE
Video zaidi

Kurasa za Haraka

  • e-Mrejesho
  • CHF ILIYOBORESHWA
  • MKATABA WA HUDUMA KWA MTEJA
  • MFUMO WA FFARS
  • MFUMO WA PLANREP
  • MFUMO WA KIBALI KUSAFIRI NJE YA NCHI

Kurasa za Mfanano

  • e-Mrejesho
  • Mkoa Morogoro
  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Jamhuri ya Muungano Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Eneo la Ramani

Wasiliana Nasi

    Halmashauri ya Wilaya Kilosa

    Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa

    Simu: 023 2623093

    Simu: 0737847880

    Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa