• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Dawati la Malalamiko |
KILOSA DISTRICT COUNCIL
KILOSA DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Idara
      • Utumishi
      • Fedha na Biashara
      • Afya
      • Mipango
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maji
      • Usafi na Mazingira
      • Mifungo na Uvuvi
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Ardhi na Maliasili
      • Ujenzi
    • Vitengo
      • sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi
      • TEHAMA
      • Uchaguzi
      • Nyuki
    • Muundo wa Halmashauri
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba Mbalimbali
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Ripoti
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Tangazo
    • Maktaba
    • Hotuba
    • Vyombo vya Habari
    • Video

WANANCHI WAHIMIZWA KUKATA KADI ZA BIMA YA AFYA - RC MORO

Posted on: October 15th, 2020

Wananchi Wilayani Kilosa na Mkoa wa Morogoro kiujumla wamehimizwa kukata kadi za bima ya afya kwa ajili ya familia zao kwani kadi hizo ni muhimu na zinasaidia kupata matibabu kwa urahisi hata nyakati ambazo mtu anakuwa hana fedha kwa ajili ya matibabu

Rai hiyo imetolewa hivi karibuni na mkuu wa Mkoa wa Morogoro Loata Ole Sanare wakati akikabidhi madawati 160 kwa shule za msingi nne,mashuka vipande 3278 na kadi za bima ya afya ICHF na NHIF vyote vikiwa vimefadhiliwa na shirika la World Vision ambalo linafanyua kazi katika Tarafa za Magole na Ulaya kupitia miradi mbalimbali katika sekta ya afya,lishe,maji,elimu na utetezi.

Licha ya kushukuru kwa ajili ya vifaa hivyo Sanare amesema kuwa Serikali inatambua misaada mbalimbali inayotolewa na World Vision lakini pia amelitaka shirika hilo kuendelea kufanya kazi na Halmashauri huku akiliomba kuongeza wigo wa kufanya kazi kwa mapana zaidi katika tarafa nyingine wilayani Kilosa na mkoa wa Morogoro.

Aidha amesema mkoa wa Morogoro umeweka mkakati wa kuwa na shule ya bweni hususani kwa shule za sekondari ili kuwalinda watoto wa kike dhidi ya vishawishi vinavyopelekea kupata mimba wakiwa shuleni na kukatisha ndoto zao ambapo ametaka kuwepo kwa ushirikiano baina ya Serikali na wazazi ili kufanikisha jambo hilo.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya Adam Mgoyi amesema shirika hilo limekuwa mdau namba moja katika kutoa misaada mbalimbali ili kupambana na umasikini ambapo wamekuwa wakitoa elimu katika shughuli mbalimbali zinazojitokeza ikiwemo kutoa elimu ya kilimo cha kisasa na cha kibiashara lakini pia wamekuwa washiriki wazuri katika kukabiliana na majanga mbalimbali kama vile janga la Corona.

Akikabidhi vifaa hivyo kwa Mkuu wa mkoa wa Morogoro kwa niaba ya shirika la World vision Meneja Mradi Elisei Chilala amesema shirika hilo limetoa madawati 160 yenye thamani ya shilingi 13,216,000,kadi za bima ya afya za ICHF kwa watoto 3,000 zenye thamani ya shilingi 15,000,000,kadi za NHIF kwa watoto 10 wenye mahitaji maalumu zenye thamani ya shilingi 504,000 na mashuka vipande 3278 kwa watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi vikiwa na thamani ya shilingi 24,585,000.

Tangazo

  • TANGAZO NAFASI ZA KAZI October 11, 2021
  • ZABUNI January 31, 2017
  • SOMA KATIBA ILIYOPENDEKEZWA March 24, 2017
  • UTARATIBU WA UHAMISHO KWA WATUMISHI WA UMMA March 24, 2017
  • Angalia zote

Habari za sasa

  • Kilosa kufanya sensa ya mifugo

    December 29, 2022
  • Kilosa kunufaika na mradi wa BOOST

    December 24, 2022
  • Kilosa yaendelea kutambua juhudi za Serikali kwa Watumishi wa Umma na Wananchi-DED Kilosa

    December 19, 2022
  • -Serikali haitosita kulinda Rasilimali watu kwa maslahi ya Maendeleo ya Taifa- Mh. Mhagama

    December 20, 2022
  • Angalia zote

Video

HIFADHII YA WANYAMA MIKUMI
Video zaidi

Kurasa za Haraka

  • CHF ILIYOBORESHWA
  • MKATABA WA HUDUMA KWA MTEJA
  • MFUMO WA FFARS
  • MFUMO WA KIBALI KUSAFIRI NJE YA NCHI
  • MFUMO WA PLANREP

Kurasa za Mfanano

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • NECTA
  • Jamhuri ya Muungano Tanzania
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Mkoa Morogoro

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Eneo la Ramani

Wasiliana Nasi

    Halmashauri ya Wilaya Kilosa

    Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa

    Simu: 023 2623093

    Simu: 0737-847-880

    Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa