Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mh. Denis Londo ametoa wito kwa wananchi wa Wilaya ya Kilosa kijiji cha Berega kata ya Berege kulitunza na kulilinda daraja ya Berega –Dumbalume linalojengwa chini ya Wakala wa Barabara za Vijijini na mijini (TARURA) amesema kukamilika kwa daraja hilo kutaondoa adha na changamoto iliyokuwepo kwa muda mrefu katika eneo hilo.
Mh Londo amesema hayo hivi karibuni akiwa pamoja na wajumbe wa Kamati hiyo wakati wa ziara ya kikazi ya kukagua maendeleo ya ujenzi unaoendelea katika daraja hilo lililopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa Mkoani Morogoro.Amesema kuwa fedha zilizotumika kujenga daraja hilo ni dhahiri kuwa Serikali imejipanga kuendelea kuwaondoa wananchi wake katika umaskini kwani uwepo wa miundombinu bora ya Barabara inarahisisha huduma za kijamii kama Hospitali,kurahisha huduma za usafiri kutoka sehemu moja kwenda nyingine
Mh Londo ametoa wito kwa viongozi wa Eneo hilo kuhakikisha wanalisimamia na kulilinda daraja hilo kwa kutoa elimu kwa Wananchi kuepuka kulima na kufanya shughuli zozote zinaweza kusababisha mmomonyoko wa udongo ambao unaweza kuharibu kingo na miundombinu ya daraja hilo.
Awali akisoma Taarifa ya mradi Mhandisi Mkazi Bw. David Mwakalalile amesema daraja hilo lina urefu wa mita 140 na upana wa mita 11 linalojengwa chini ya Mkandarasi Nyaza Road Works Limited Mwanza litagharimu shilingi Bilioni 7.9 na amesema atasimamia mradi huo kwa ubora na kukamilika kwa wakati
Kwa upande wa Mbunge wa Jimbo la Kilosa Mhe. Profesa Palamagamba Kabudi ameishukuru Serikali ya Awamu ya sita inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa uwekezaji mkubwa kwa wananchi sio tu kwa usafirishaji wa biashara zao lakini pia kutatua changamoto zilizokuwa zinatokea kwani wapo watu waliopoteza maisha kabla ya kuwepo kwa daraja hilo.
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa