• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Dawati la Malalamiko |
KILOSA DISTRICT COUNCIL
KILOSA DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Divisheni
      • Utawala,Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Viwanda,Biashara na Uwekezaji
      • Huduma za Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Mipango na Uratibu
      • Elimu ya Awali na Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Miundombinu ya Mijini na Vijijini
    • Vitengo
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Usimamizi na Ununuzi
      • TEHAMA na Takwimu
      • Fedha na Uhasibu
      • Maliasili na Mazingira
      • Mawasiliano Serikalini
        • Michezo,Utamaduni na Sanaa
      • Michezo,Utamaduni na Sanaa
      • Usimamizi wa Taka Ngumu na Usafi wa Mazingira
    • Muundo wa Halmashauri
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba Mbalimbali
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Ripoti
    • Jarida la Mtandaoni
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Tangazo
    • Maktaba
    • Hotuba
    • Vyombo vya Habari
    • Video

WATENDAJI WA KATA WATAKIWA KUSIMAMIA MAPATO NA MIRADI UFANISI

Posted on: November 12th, 2024

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa, akizungumza katika kikao kazi cha watendaji wa kata kilichofanyika leo katika ukumbi wa Halmashauri hiyo, amewataka watendaji hao kusimamia kwa umakini na ufanisi miradi yote ya maendeleo katika maeneo yao. Amesema watendaji wanapaswa kuwa mstari wa mbele kuhakikisha kuwa miradi inatekelezwa kwa wakati na viwango vinavyotarajiwa ili kufanikisha lengo la serikali la kuwaletea wananchi maendeleo endelevu.

Mkurugenzi Mtendaji amesisitiza kwamba usimamizi thabiti wa miradi ni msingi wa kuleta mabadiliko chanya kwa jamii, huku akieleza kuwa watendaji wanapaswa kuibua na kuzitolea taarifa changamoto zinazojitokeza mapema. “Changamoto zinazotokea kwenye miradi lazima zifahamike mapema ili hatua zichukuliwe mara moja,” alisema. “Kazi ya mtendaji sio tu kuratibu miradi, bali kuhakikisha inafikia malengo yake kwa viwango vilivyokusudiwa. Tunataka kuona kuwa fedha za umma zinatumika kwa manufaa ya kweli kwa wananchi na si vinginevyo.”

Akiendelea na maelekezo yake, Mkurugenzi aliwataka watendaji wa kata kutambua kuwa jukumu la kusimamia miradi linaenda sambamba na kuwajibika kwa ufanisi wa vyanzo vya mapato vya halmashauri. Amesema ni muhimu kwa watendaji kuainisha na kutambua vyanzo vya mapato vilivyopo katika maeneo yao ambavyo bado havijafikiwa au kutumiwa kikamilifu na serikali. “Lazima tuwe wabunifu katika kutafuta na kuongeza mapato ya halmashauri kwa kutumia vyanzo vyote vilivyopo,” alieleza Mkurugenzi, akiongeza kuwa mapato hayo ni muhimu kwa kuboresha huduma mbalimbali zinazotolewa kwa wananchi.

Kwa upande wake, Afisa Utumishi wa halmashauri aliwataka watendaji wa kata kuhakikisha mapato yanayokusanywa na vijiji yanaingizwa benki ili kupunguza mianya ya uvujaji wa mapato na kuongeza uwazi katika ukusanyaji huo. Aliwahimiza pia kusimamia wenyeviti wa vijiji kuwajibika kwa kuitisha mikutano ya mara kwa mara kwa mujibu wa sheria, hatua ambayo inasaidia wananchi kufuatilia matumizi ya mapato yao. Afisa huyo aliwahimiza watendaji kuhuisha sheria ndogondogo za vijiji ili ziwasaidie kuwaongoza na kuhakikisha matumizi sahihi ya mapato ya vijiji kwa manufaa ya wananchi.

Kikao hicho kilimalizika kwa watendaji wa kata kuonesha nia ya kuyatekeleza maagizo yaliyotolewa, wakiapa kufanya kazi kwa bidii na kujituma katika kuhakikisha miradi ya maendeleo na ukusanyaji wa mapato unafanyika kwa mafanikio na matokeo yanayoonekana.

Tangazo

  • TANGAZO LA KONGAMANO LA VIJANA WILAYANI KILOSA April 04, 2025
  • Tangazo la kuanzishwa Dawati Maalum la kushughulikia Migogoro ya Wakulima na Wafugaji November 13, 2024
  • Tangazo la Dawati la Msaada wa Kisheria November 13, 2024
  • TANGAZO LA BARAZA LA MADIWANI LA RISIMU NA MAPENDEKEZO YA MPANGO NA BAJETI KWA MWAKA WA FEDHA 2025/2026 February 25, 2025
  • Angalia zote

Habari za sasa

  • VIONGOZI WA VYAMA VYA SIASA WAMETAKIWA KUHAMASISHA WANANCHI KUBORESHA TAARIFA ZAO

    May 07, 2025
  • RC MALIMA AWATAKA WAAJIRI MOROGORO KUTATUA CHANGAMOTO ZA WATUMISHI WAO

    May 01, 2025
  • WALIMU WAPYA 74 WILAYANI KILOSA WAPEWA MAFUNZO ELEKEZI KUHUSU MAADILI NA HAKI ZA UTUMISHI WA UMMA

    April 29, 2025
  • KILOSA YABORESHA USIMAMIZI NA UFATILIAJI WA MIKOPO YA 10% KWA UNUNUZI WA GARI JIPYA

    April 29, 2025
  • Angalia zote

Video

RAIS SAMIA ATENGA BILIONI 7.2 KUENDELEZA BONDE LA RUHEMBE
Video zaidi

Kurasa za Haraka

  • e-Mrejesho
  • CHF ILIYOBORESHWA
  • MKATABA WA HUDUMA KWA MTEJA
  • MFUMO WA FFARS
  • MFUMO WA PLANREP
  • MFUMO WA KIBALI KUSAFIRI NJE YA NCHI

Kurasa za Mfanano

  • e-Mrejesho
  • Mkoa Morogoro
  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Jamhuri ya Muungano Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Eneo la Ramani

Wasiliana Nasi

    Halmashauri ya Wilaya Kilosa

    Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa

    Simu: 023 2623093

    Simu: 0737847880

    Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa