• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Dawati la Malalamiko |
KILOSA DISTRICT COUNCIL
KILOSA DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Divisheni
      • Utawala,Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Viwanda,Biashara na Uwekezaji
      • Huduma za Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Mipango na Uratibu
      • Elimu ya Awali na Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Miundombinu ya Mijini na Vijijini
    • Vitengo
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Usimamizi na Ununuzi
      • TEHAMA na Takwimu
      • Fedha na Uhasibu
      • Maliasili na Mazingira
      • Mawasiliano Serikalini
        • Michezo,Utamaduni na Sanaa
      • Michezo,Utamaduni na Sanaa
      • Usimamizi wa Taka Ngumu na Usafi wa Mazingira
    • Muundo wa Halmashauri
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba Mbalimbali
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Ripoti
    • Jarida la Mtandaoni
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Tangazo
    • Maktaba
    • Hotuba
    • Vyombo vya Habari
    • Video

WATUMISHI WA KADA MBALIMBALI ZA HALMASHAURI WAPATIWA MAFUNZO YA MFUMO WA NEST

Posted on: June 9th, 2025

Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Mhe. Shaka Hamdu Shaka amefungua rasmi mafunzo ya mfumo wa manunuzi yaani (NEST), kwa watendaji wa Kata na Vijiji, Walimu, pamoja na Waganga wafawidhi wa vituo vya afya vilivyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa na kuwataka watumishi  hao kuutumia mfumo huo ipasavyo kwani Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ina dhamira kubwa ya kuendeleza miradi iliyopo katika Halmashauri kwa kutangaza tenda kupitia mfumo huo wa Manunuzi.

Shaka ameyasema hayo  June 09, 2025 katika Ukumbi wa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi  (FDC-ILONGA) alipokuwa akitoa hotuba yake iliyojikita katika kutoa pongezi kwa Mamlaka ya udhibiti wa manunuzi ya umma (PPRA) Kwa kutengeneza mfumo wa manunuzi kwa njia ya kielekroniki unaojulikana kama NEST na kuusimamia vyema kwa ajili ya kuleta tija na ufanisi katika kurahisisha kuweka uwazi, uwajibikaji na kupunguza mianya ya rushwa katika ununuzi unaofanywa na taasisi za umma.

Naye Bwana Emmanuel Telya ni Afisa mwandamizi kutoka Mamlaka ya udhibiti wa manunuzi ya umma (PPRA) amesema kuwa lengo mahususi ya kufanya mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo  watumishi wa Halmashauri pamoja na watumishi kutoka katika vituo vya kutolea huduma ngazi za Shule za msingi pamoja na Shule za sekondari, vituo vya afya pamoja na Watendaji wa Kata na Vijiji,ili kuwaongezea ufanisi  na weredi katika matumizi ya Mfumo huo wa Manunuzi  kwa njia ya kielekroniki yaani NEST.

Grace Nyabange ni msimamizi wa Kitengo cha Ununuzi na Ugavi katika Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa nae ameweza kuzungumza machache juu ya mafunzo yaliyotolewa na PPRA kwa watumishi wa umma,ambapo amesema kuwa mafunzo hayo wameanza kwa Watumishi wa ngazi za chini yaani Low level ikiwahusisha Wakuu wa Shule za msingi na Sekondari  na wasaidizi wao, Waganga wafawidhi wa vituo vya afya na Zahanati na wasaidizi wao pamoja na Watendaji wa Kata na Vijiji katika Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa.

Bwana Godwik Edward ni Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Mvumi Kata ya Mvumi akiwa mmoja wapo wa watumishi waliopata mafunzo hayo nae amesema kuwa amefurahishwa sana na mafunzo hayo ya mfumo wa manunuzi kwa njia ya Kielekroniki kwani yamempa uwezo wa kuweza kufanya manunuzi kupitia mfumo huo wa wazi kwani kipindi kilichopita walikuwa wanapata shida hasa katika mfumo huo  ulipokuwa bado haujaanza.

Naye Mwl. Hidath kutoka Shule ya Sekondari Gongo yeye ni Mwalimu wa Manunuzi katika Shule hiyo yeye amesema kuwa mafunzo hayo yanawasaidia kwa namna nyingi tofauti na zamani walipokuwa wanatumia mfumo wa kawaida. Mfumo wa NEST umekuja kurahisisha manunuzi kwa sababu ni mfumo ambao haupati shida ya kuzunguka kutangaza tenda ili umpate mzabuni wa kuchagua.

Mamlaka ya udhibiti wa Manunuzi ya Umma PPRA imerahisisha manunuzi ya umma kwa kuleta mfumo huo kwa njia ya Kielekroniki yaani NEST kwa Halmashauri zote nchini kwa lengo la kuweka wazi na uwajibikaji pamoja na kubaini vitendo vya rushwa vinavyofanyika katika vitengo vya Manunuzi

Tangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI KILOSA DC June 06, 2025
  • Tangazo la kuanzishwa Dawati Maalum la kushughulikia Migogoro ya Wakulima na Wafugaji November 13, 2024
  • Tangazo la Dawati la Msaada wa Kisheria November 13, 2024
  • TANGAZO LA BARAZA LA MADIWANI LA RISIMU NA MAPENDEKEZO YA MPANGO NA BAJETI KWA MWAKA WA FEDHA 2025/2026 February 25, 2025
  • Angalia zote

Habari za sasa

  • DC SHAKA AWATAKA VIONGOZI WA VIJIJI KUCHUKUA HATUA DHIDI YA VITENDO VYA UVUNJIFU WA AMANI KIDUHI

    June 19, 2025
  • DC SHAKA AWATAKA VIONGOZI NGAZI YA KATA NA VIJIJI KUSIMAMIA NA KUFUATILIA MIRADI YA MAENDELEO IPASAVYO

    June 19, 2025
  • DC SHAKA AWATAKA WAZAZI / WALEZI KUWAJIBIKA KATIKA MALEZI BORA YA WATOTO

    June 16, 2025
  • TIMU YA MENEJIMENTI KILOSA YAFANYA ZIARA YA KUTEMBELEA NA KUKAGUA MIRADI YA MAENDELEO

    June 12, 2025
  • Angalia zote

Video

RAIS SAMIA ATENGA BILIONI 7.2 KUENDELEZA BONDE LA RUHEMBE
Video zaidi

Kurasa za Haraka

  • e-Mrejesho
  • CHF ILIYOBORESHWA
  • MKATABA WA HUDUMA KWA MTEJA
  • MFUMO WA FFARS
  • MFUMO WA PLANREP
  • MFUMO WA KIBALI KUSAFIRI NJE YA NCHI

Kurasa za Mfanano

  • e-Mrejesho
  • Mkoa Morogoro
  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Jamhuri ya Muungano Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Eneo la Ramani

Wasiliana Nasi

    Halmashauri ya Wilaya Kilosa

    Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa

    Simu: 023 2623093

    Simu: 0737847880

    Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa