Katibu wa Chama cha Wauguzi Mkoa wa Morogoro Ndg. Awadhi Juma amewataka wauguzi wote wa Mkoa wa Morogoro kufanya kazi kwa wito na kuacha kuweka mbele maslahi yao binafsi kwani kufanya hivyo ni kukiuka maadili ya kazi lakini pia kutofanya upendeleo kwani wagonjwa wote wanastahili huduma sawa.
Awadhi amezungumza hayo katika hafla ya kuadhimisha siku ya wauguzi duniani iliyofanyika Mei 30, 2025 katika Hospitali ya Wilaya ya Kilosa ambapo wauguzi wa hospitali hiyo wameadhimisha siku hiyo kwa kufanya maandamano katika eneo la hospitali huku wakitembelea wagonjwa na kuwapitia zawadi katika wodi zote.
Katibu huyo amesema kuwa kila muuguzi awajibike kwa nafasi yake na kwa atakayekiuka na kwenda kinyume na maadili ya kazi hatua kali za kinidhamu zitachukuliwa dhidi yake.
Katika Hafla hiyo Wauguzi hao wamesema kuwa kufanya sherehe hizo ni sehemu moja wapo ya kumbukumbu ya kuyaenzi mema ya muanzilishi na muasisi wa huduma ya wauguzi wataaluma ya ukunga duniani ndugu frolensi Naitingali ambapo alikuwa akitoa huduma ya wito nakujali majeruhi nchini ufaransa mwaka 1800 bila malipo yoyote na alifanya kazi kwa weredi wa hali ya juu.
Hafla hiyo ilienda sambamba na uapisho ambapo wauguzi hao waliweza kula kiapo cha utii mahali pa kazi.
Sherehe hizo ufanyika kila mwaka ifikapo tarehe 12 mwezi Mei huku Kitaifa yakiadhimishwa Mkoani Iringa.
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa