SURA NA TASWIRA YA HALMASHAURI
1.0 UTANGULIZI:
Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa ni miongoni mwa Halmashauri tisa za Mkoa wa Morogoro. Halmashauriilianzishwa mnamo tarehe 25 Agosti,1962 chini ya kifungu 6 (1) cha Sheria za Serikali za Mitaa Sura 333. Baada ya kuvunjwa wakati wa kipindi chaMadaraka Mikoani mwaka 1972, Halmashauri ilirejeshwa tena mwezi Januari 1982.
Halmashauriina eneo lenye kilometa za mraba 14,245 sawa na 19.5% ya eneo lote la Mkoa wa Morogoro. Halmashauri inatekelezamajukumu yake katika Wilaya za Kilosa naGairo kufuatia kuanzishwa kwa Wilaya ya Gairo kwa Tangazo la Serikali Na. 73 latarehe 01 Machi, 2012. Hivi sasa Wilaya ya Kilosa ina eneo la kilometa za mraba12,393.7 na Wilaya ya Gairo kilometa za mraba 1,851.3 pekee.
Halmashauriipo kati ya “Latitude” 5o 55’ na 7o 53’ Kusini mwa Ikwetana “Longitude” 36o 30’ na 37o 3’ Mashariki mwaGriniwichi. Halmashauri inapakana naHalmashauri ya Wilaya ya Mvomerokwa upande wa Mashariki na upande wa Kusini inapakana na Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero na Mkoa wa Iringa. Kwa upande waKaskazini inapakana na Mikoa ya Manyara (Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto) naTanga (Halmashauri ya Wilaya ya Kilindi), na Magharibi inapakana na Halmashauri za Wilaya za Mpwapwa na Kongwazilizopo Mkoa wa Dodoma.
2.0 IDADIYA WATU:
Kutokanana Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2002 Halmashauri ilikuwa na wakazi 489,513(Me 244,201 na Ke 245,312) sawa na watu 34 kwa kilomita ya mraba na sawa na27.8% ya wakazi wote wa Mkoa wa Morogoro. Kwa mwaka 2012 Halmashauri inakadiriwakuwa na watu wapatao 596,434 ambapo wanaume ni 289,774 na wanawake ni 292,102sawa na ongezeko la kila mwaka 2.5%. Halmashauri ilikadiriwa kuwa na kaya 105,635 zenye wastani wa idadi yawatu 4.6 kwa kila kaya.
3.0 MUUNDO WAUTAWALA WA HALMASHAURI:
Halmashauriina tarafa tisa za Mikumi, Gairo, Ulaya, Masanze, Kimamba, Nongwe, Kidete,Magole na Kilosa Mjini. Tarafa hizo zinagawanyika katika Kata 46, Vijiji 164 naVitongoji 1,040. Halmashauri inaMajimbo matatu ya Uchaguzi na Mamlaka za Miji Midogo mitatu ya Gairo, Kilosa naMikumi. Serikali imeshatoa Notisi ya kuanzisha Halmashauri ya Wilaya ya Gairokwa Tangazo la Serikali Na. 28 la tarehe31 Agosti 2012.
Halmashauriinapaswa kuwa na jumla yaWaheshimiwa Madiwani 65 wakiwemo Waheshimiwa Wabunge watatu, WaheshimwaMadiwani wa Kata 46 na Waheshimiwa Madiwani viti maalumu 16. Katika Baraza laMadiwani, kuna Waheshimiwa Madiwani wanawake 19 wakiwemo watatu wa kuchaguliwasawa na 30.6% ya wajumbe. Hata hivyo kwa sasa idadi ya Waheshimiwa Madiwani ni61 baada ya aliyekuwa Diwani wa Kata ya Masanze, Mhe. Diwani Leonard M. Mapunda, kufariki tarehe 05 Julai2012.
Aidhakuna jumla ya vyama 11 vya siasa ambavyo ni CCM, SAU, CUF, UDP, NCCR MAGEUZI, JAHAZI ASILIA, CHADEMA, DEMOKRASIAMAKINI, UMD, UPDP na TLP vilivyoshirikikatika Uchaguzi Mkuu uliofanyika tarehe 31 Oktoba 2010. Waheshimiwa Madiwaniwote wanatokana na CCM isipokuwa wawili ambao ni wa CHADEMA.
Kwakuzingatia muundo wa Halmashauri ulioidhinishwa na Waziri mwenye dhamana yaSerikali za Mitaa kwa Waraka Kumb. Na. GA 215/262/0183 wa tarehe 25 Juni, 2012Halmashauri inazo Idara 13 na vitengo sita kama ilivyo katika jedwali Na. 1.
Kwamujibu wa Ikama ya mwaka 2011/12, Halmashauri ina jumla ya watumishi 4,135 kamailivyoainisha katika jedwali lifuatalo.
Jedwali Na:2 Ikama ya watumishi 2011/2012
SN
|
KADA
|
IDADI
|
1
|
Utumishi na Utawala
|
226
|
2
|
Fedha na Biashara
|
30
|
3
|
Elimu ya Sekondari
|
597
|
4
|
Elimu ya Msingi na Utamaduni
|
2251
|
5
|
Ardhi na Maliasili
|
32
|
6
|
Afya
|
619
|
7
|
Usafi na Mazingira
|
16
|
8
|
Maendeleo ya Jamii,Ustawi wa Jamii na Vijana
|
66
|
9
|
Maji
|
51
|
10
|
Ujenzi
|
48
|
11
|
Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
|
9
|
12
|
Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
|
139
|
13
|
Mifugo na Uvuvi
|
51
|
|
JUMLA
|
4,135
|
KatikaIkama ya mwaka 2012/13 Halmashauri imeomba kuidhinishiwa watumishi 870 iliiweze kutimiza malengo yake kwa ufanisi zaidi.
4.0 DIRA,DHAMIRA NA MALENGO YA HALMASHAURI:
Kwamujibu wa Mpango Mkakati wa Halmashauri 2010 - 2015, Dira ya Halmashauri ni “Maisha bora kwa wote”, na dhamira yaHalmashauri ni “Kuipatia jamii huduma namaisha bora kwa kuijengea mazingira mazuri ya ushiriki katika kuleta maendeleoendelevu ya kijamii na uchumi katika Wilaya ya Kilosa”.
Katikakutimiza dhamira yake, Halmashauri imejiwekea malengo makuu manane ambayo ni:
1. Kuboreshahuduma ya UKIMWI na kupunguza maambukizi mapya.
2. Kuboresha,kuendeleza na kutekeleza kikamilifu Mpango wa Taifa wa Kupambana na Rushwa.
3. Kuimarishaushiriki wa jamii na watu binafsi katika kupanga, kusimamia na kutekelezashughuli za maendeleo.
4. Kuendelezahuduma za kiuchumi na miundombinu.
5. Kuimarishautawala bora na utumishi wa umma katika kuleta maendeleo.
6. Kuimarishana kuendeleza shughuli za maliasili nakudhibiti uharibifu wa mazingira.
7. Kuendelezana kujumuisha masuala mtambuka yakiwemo ustawi wa jamii.
8. Matayarishoya kujikinga na majanga pamoja na masuala ya dharura.
Halmashauriinao mpango mkakati wa miaka mitano (2010 – 2015).
5.0 HUDUMAZA KIUCHUMI:
5.1 SEKTA YA KILIMO, UMWAGILIAJI NA USHIRIKA:
5.1.1 Kilimo:
Asilimia 88 ya wakazi wa Halmashauri hiihutegemea kilimo kama njia ya kujipatia mapato na chakula. Malengo ya kilimo kwa msimu uliopita2011/12 yalikuwa kulima jumla ya hekta 249,618 zikiwemo 206,113 za mazao yachakula na hekta 43,505 za mazao ya biashara. Hali halisi ya utekelezaji nikwanba jumla ya hekta 188,919 zililimwa, zikiwemo hekta 158,231 za mazao yachakula na hekta 30,688 za mazao ya biashara.
Aidha matarajioya mavuno kwa mazao ya chakula yalikuwa ni kuvuna tani 739,712. Kwa mazao yachakula na kwa mazao ya biashara yalikuwa ni kuvuna tani 918,138. Hadi mwishowa wakati wa mavuno jumla ya tani 478,381 za mazao ya chakula na tani 720,235 ya biashara zilivunwa.
Utekelezaji wa shughuli za kilimo umezingatiamaagizo ya Serikali katika kutekeleza Tamko la Kilimo Kwanza na “Fanya Mkoa waMorogoro kuwa Ghala la Taifa” (FAMOGATA). Shughuli mbalimbali zimefanyikakatika kufikia azma hiyo.
Miongonimwa Shughuli zilizotekelezwa ili kufikia azma hiyo ni:
a) Kuendeleza uzalishaji wa mazao ya chakula nabiashara.
b) Uzalishaji mbegu daraja la kuazimiwa ubora katikavijiji vya Msimba, Malolo, Mwasa, Madudu na Kimamba.
c) Uboreshaji wa skimu za umwagiliaji kwa ujenzi wamifereji mikuu ya Mwasa (meta 200), Madizini (meta 200), Chanjale (meta 200),Mvumi (meta 2,750 na kalvati 20), Ilonga (meta 2,000 na kalavati 8) na Msowero(meta 2,500 na kalavati 8) pamoja na Mwega kirusha maji (meta 300 x 25).
d) Vikundi vitano vya Mtumbatu, Magubike, Mvumi, RudewaGongoni na Ihombwe vimepewa majembe ya wanyamakazi aina ya Mkombozi, pea mbiliza maksai na mkokoteni kila kijiji. Pia Wilaya imepokea trekta mpya tatu kutokaSUMA JKT aina ya farmatrack 60 (50 HP2WD) walizokopeshwa wakulima.
Aidha kupitia Serikali Kuu zoezi la kusambazavocha za pembejeo za ruzuku liliendelea kufanyika. Katika mwaka 2011/2012 Halmashauriilipata jumla ya vocha 90,776 kama ifuatavyo:
Mapokeziya vocha za pembejeo yalikuwa kama ifuatavyo:
(a) Mbolea ya kupandia –Vocha 30,242
(b) Mbolea ya kukuzia – Vocha 30,242
(c) Mbegu (OPV) – Vocha 9,800
(d) Mbegu (Chotara) – Vocha 18,642
(e) Mbegu (Mpunga) –Vocha 1,800
Hatahivyo jumla ya vocha DAP 3,080; UREA 3,079; OPV 2,906; na chotara 90hazikutumika na zilirudishwa Wizarani.
Uanzishaji waMazao Mapya:
Wilayaimeanzisha uzalishaji wa zao jipya la kakao katika Kijiji cha Kisongwe natangawizi katika kijiji cha Lumbiji. Hatua iliyofikiwa kwa sasa ni uzalishajiwa tani 96 la zao la tangawizi.
5.1.2 Umwagiliaji:
Hadi sasa eneo lililoboreshwa kwaajili ya umwagiliaji ni hekta 11,000 kati ya hekta 32,000 zinazofaa kwaumwagiliaji.
5.1.3 Ushirika:
Halmashauriina jumla ya Vyama vya Kuweka na Kukopa 55 na Vyama vingine vya Ushirika 21.Wananchi wameendelea kuhamasishwa kujiunga na SACCOS pamoja na vyama vinginevya ushirika. Katika kipindi cha 2011/2012 jumla ya watu 11,827 (Me 7493 na Ke4334), vikundi 298 na taasisi 34 zilijiungana SACCOS na kufanya jumla ya wanachama kuwa 12,159 mwaka 2011. Halmshauri ilitekeleza pia zoezi la uanzishaji wa SACCOS kwa kilaKata kwa 92% na iliendelea na uhamasishaji kwa wananchi ili waendelee kujiunga.
Aidha katika Mpango wa Uwezeshaji waWananchi Kiuchumi na Kukuza Ajira, SACCOS sita zilifanikiwa kupata mikopo yenye thamani ya Tsh. 537,000,000kutoka CRDB; SACCOS nne kupitia Akiba Commercial Bank (Tsh. 79,000,000.00) na jumlaya wajasiriamali 94 walipata mkopo kupitia NMB (T.Shs:67,120,000.00).
5.2 SEKTA YA MIFUGO NA UVUVI:
5.2.1 Mifugo:
Ufugajini shughuli muhimu inayoendelea katika Halmashauri. Halmashauri ina hekta483,390 zinafaa kwa malisho. Wanyamawafugwao ni wa asili ambao wanakisiwa kuwa ng’ombe 211,610; mbuzi 92,579;kondoo 24,357; nguruwe 4,917; kuku 500,612; punda 2,941; na sungura 1,201.
Mifumoya ufugaji inayoendeshwa ni ya aina tatu:-
a) Ufugaji huria ambao ndiyo mkubwa kwa kundi la ufugaji wa asili katikaTarafa za Magole, Kimamba na Masanze.
b) Ufugaji mchanganyiko wa mifugo ya asili na kilimocha mazao katika tarafa za Gairo, Nongwe na sehemu ya magharibi ya Tarafa zaMagole, Kidete na Mikumi.
c) Ufugaji wa ndani wa ng’ombe na mbuzi wa kisasa wa maziwa na nguruwe katika Tarafa ya KilosaMjini, Kimamba, Ulaya, Mikumi, Magole/Gairo, Kidete na Masanze.
Katikakuendeleza ufugaji shughuli mbalimbali zimeendelea kutekelezwa zikiwemo:
a) Kuongezathamani ya mazao ya mifugo na kuhamasisha ufugaji endelevu kwa kutumia madumebora, uhamilishaji na kutoa chanjo.
b) Kuimarishamiundombinu ya mifugo na kutoa huduma za ugani kwa kuendeleza ujenzi wamiundombinu kama jedwali hapa chinilinavyoonesha.
Miundombinu ya Mifugo
Na
|
Miundombinu
|
Hitaji
|
Vilivyopo
|
Pungufu
|
1
|
Majosho
|
164
|
46
|
118
|
2
|
Minada
|
13
|
7
|
6
|
3
|
Vituo vya Afya ya Mifugo
|
37
|
4
|
33
|
4
|
Vibanio
|
55
|
5
|
50
|
5
|
Machinjio Makubwa
|
10
|
6
|
4
|
6
|
Mabanda ya ngozi
|
10
|
2
|
8
|
7
|
Mabwawa/ Malambo
|
46
|
8
|
38
|
c) Kutenga maeneo ya wafugaji ili kupunguza migogorokwa kuanzisha vijiji vya wafugaji ingawa vijiji vingine zaidi vina mchanganyikowafugaji na wakulima.
5.2.2 Uvuvi:
Uvuvikatika Halmashauri hufanywa katika mitomikuu 10, mabwawa ya asili na yale yaliyochimbwa na watu binafsi. Kuna jumla yamabwawa 155 ya kuchimbwa na jumla ya vifaranga 30,000 vya samaki vilisambazwakwa wananchi katika kipindi cha 2011/2012 ukilinganisha na vifaranga 10,000 mwaka 2005/06
5.3 SEKTAYA ELIMU:
5.3.1 Elimuya Awali:
Katika mwaka 2011/2012 Halmashauriilikuwa na jumla madarasa ya elimu ya awali 185 yenye jumla ya watoto 10,969. Katiyao wavulana walikuwani 5,542 na wasichana 5,427. Madarasahayo yapo katika Shule za Msingi 185 ambapo shule 34 hazina madarasa ya awali. Niaya Halmashauri ni kufanya kila shule ya msingi iwe na darasa la awali.
Idadi ya shule zenyemadarasa ya Awali.
Mwaka |
Jumla ya shule zote |
Shule zenye madarasa ya awali |
Shule zisizo na madarasa ya awali |
Idadi ya wanafunzi wa awali |
||
WAV |
WAS |
JML |
||||
2011/12 |
219 |
185 |
34 |
5,542 |
5,427 |
10,969 |
5.3.2 Elimuya Msingi:
a) Usajiliwa wanafunzi Darasa I hadi VII:
Miongoni mwa majukumumakuu ya Halmashauri ni kutoa huduma ya elimu ya msingi kwa wananchi wake nakuboresha huduma hiyo. Katika mwaka 2011/2012, Halmashauri ilikuwa na Shule zaMsingi 229 ambapo kati ya hizo 219 ni za serikali na shule tatu ni za binafsi. Shule za serikali zilikuwa na jumla yawanafunzi 103,989 kati yao wasichana ni 53,683 na wavulana ni 50,306 na shule za binafsi zilikuwa na jumla ya wanafunzi 691 ambapokati yao wavulana ni 331 na wasichana 360.
b) Uandikishaji wa wanafunzi wa darasa lakwanza:
Katika mwaka 2012Halmashauri ilifanikiwa kuandikisha jumla wa wanafunzi wa darasa la kwanza 16,617kati yao wasichana 8,374 na wavulana 8,245 sawa na asilimia 98.5 ya lengo lakuandikisha wanafunzi 16,870.
b) Haliya Walimu:
Halmashauri ina jumla yawalimu 2,213 ikiwa na upungufu wa walimu 386 kulingana na mahitaji ya walimu 2,599.Uwiano wa mwalimu kwa mwanafunzi nimwalimu mmoja kwa wanafunzi 48 (1:48)
c) Hali ya Majengo nasamani:
Kwa mwaka 2011/2012 Halmashauriilikuwa na vyumba vya madarasa 1,391 kati ya mahitaji ya madarasa 2,599 kukiwana upungufu wa madarasa 1,124 sawa na asilimia 43.0 ya mahitaji. Vilevile Halmashauriilikuwa na nyumba za walimu 442 kati ya mahitajiya nyumba 2,213 kukiwa na upungufu wa nyumba 1.771 sawa na asilimia 80 yamahitaji. Aidha Halmashauri ilikuwa na matundu ya choo 1,913 kati ya mahitajiya matundu 5,050 kukiwa na upungufu wa matundu ya vyoo 3,137 sawa na asilimia 62.4ya mahitaji yote. Aidha kwa upande wa samani Halmashauri ilikuwa na madawati 27,397kati ya mahitaji ya madawati 46,321 kukiwa na upungufu wa madawati 5,424 sawana alilimia 34.0 ya mahitaji.
d) Haliya Vifaa vya kufundishia na kujifunzia:
Katika kukabiliana natatizo la vifaa vya kufundishia na kujifunzia, Halmashauri ilinunua Vivunge 206vya mwili wa binadamu, Vivunge 210 vya hesabati na matufe ya ramani ya Dunia1,470 kupitia mpango wa MMEM. Hata hivyo, juhudi za kupunguza tatizo hilo zinafanyika kwakuhakikisha kuwa kiasi cha fedha kinatengwa kwenye bajeti kwa ajili ya kununuliavifaa vya kufundishia na kujifunzia.
e) Uwianowa vitabu kwa wanafunzi:
Halmashauri bado ina upungufu mkubwa wa vitabu mashuleni.Kwa wastani uwiano ni 1:4 ambapo sera inasema kuwa uwiano uwe 1:1.
f) Hali ya Taaluma:
Hali ya taaluma kiwilayaimepanda. Hii inatokana na jitihada zilizofanyika kwa mazingira ya kufundishiana kujifunzia ambapo hali ya ufaulu kuanzia mwaka 2009 ni kamaifuatavyo:
Mwaka
|
Waliofanya mtihani
|
Waliofaulu
|
%
|
||||
|
Me
|
Ke
|
Jumla
|
Me
|
Ke
|
Jumla
|
|
2009
|
6434
|
7161
|
13595
|
3400
|
3135
|
6535
|
48.1
|
2010
|
5264
|
6074
|
11338
|
3024
|
6231
|
9255
|
54.96
|
2011
|
6613
|
7339
|
13952
|
3486
|
7063
|
10549
|
50.6
|
5.3.3 Elimu ya Sekondari:
Kwa mwaka 2011/2012 Halmashauriilikuwa na Shule 51 za Sekondari. Kati ya hizo Shule 47 ni za Serikali na shulenne zinamilikiwa na watu binafsi. Katika shule hizi wapo wanafunzi 17,541 kati yao wasichana ni 9,351 nawavulana ni 10,190. Aidha, walimu waliopo ni 625 kati yaowalimu wa kike ni 95 na walimu wa kiume ni 526 ambapo mahitaji ya walimu katikashule za sekondari hadi Juni, 2012 ni kamailivyo katika jedwali:
Mahitaji
|
Waliopo
|
|
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa