HATUA ZA KUCHUKUA ILI KUPATA HATI YA HAKIMILIKI (TITTLE DEED) MJINI
1.Eneo husika lazima liwe limetangazwa kuendelezwa kimipango miji(Planning areas).
2.Eneo liwe limeandaliwa michoro ya Mipango Miji na kusajiliwa wizarani.
3.Eneo liwe limepimwa kwa kufuata mchoro wa mpango mji uliopo na kupata usajili kwa Ramani hiyo ya upimaji wizarani.
4.Baada ya hapo taratibu za kuomba kumilikishwa kiwanja/eneo lako zinafuata kwa kujaza fomu ya maombi ya kiwanja(Land Form Na 19).
5.Ukisha kubaliwa maombi ya kupata kiwanja utatakiwa kulipia gharama ya kiwanja husika(Plot price) amabayo itategemeana na ukubwa na matumizi ya kiwanja.
6.Baada ya kulipia kiwanja utaandikiwa nyaraka ya Ankara ya malipo ya gharama za HATI (Tittle costs) katika kiwanja chako. Gharama hizi ni pamoja na:
a)Premium fee.
Hii inatozwa 7.5% ya thamani ya kiwanja (Land Value)
b)Registration Fee.
Hii inatozwa 20% ya kodi ya ardhi ya mwaka(Annual Land Rent) Mfano kodi ya mwaka ya kiwanja ni 20,000/=, RF=20,000/= X 0.2=4000/=
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa