Halmashauri ya wilaya ya kilosa imefanikiwa kuchanja mbwa wengi dhidi ya ugonjwa wa kichaa cha mbwa katika kampeni maalumu ya wiki ya kichaa cha mbwa ambayo kilele chake kimefanyika katika kijiji cha Kitete Msindazi kata ya Ruhembe.
Hayo yamesemwa Septemba 28, 2025 na Afisa Mifugo kutoka ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa Devid Shemweta wakati wa kuitimisha kampeni hiyo na kufafanua kuwa Halmashauri ilipokea dozi 550 za chanjo ya ruzuku kutoka wizara ya mifungo ambapo katika kipindi hiki cha wiki ya chanjo ya kichaa cha mbwa imetolewa bure.
Shemweta ameongeza kuwa kampeni hiyo imehusisha utoaji wa elimu juu ya ufugaji bora wa mbwa katika maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja na namna bora ya kutunza na kuwahudumia mbwa lakini pia namna ya kuwakinga dhidi ya magonjwa
Aidha ameiomba serikali kuendelea kutoa chanjo hizo kwani bado mahitaji ni makubwa kwani chanjo zilizotolewa haziwezi kukidhi idadi ya mbwa na paka wote waliopo kwenye Halmashauri nzima.
Katika hatua nyingine, amewataka wafugaji wa mbwa kuwa makini na mbwa wao kwani maeneo mengi ya wilaya ya Kilosa yamepana na Mbuga za wanyama na magori hiyo ni rahisi kwa wanyamapori kuchangamana na wale wafugwao jambo ambalo linaweza kusabisha ugonjwa wa kichaa cha mbwa.
Kwa upande wao baadhi ya wafugaji waliojitokeza kuchanja mbwa wao, wameishukuru serikali kwa kuleta chanjo hiyo bure huku wakitoa wito kwa wale ambao hawajapata huduma hii kuwaleta mbwa na paka wao kupata chanjo.
Maadhimisho haya ya chanjo ya Kichaa cha mbwa ya mebebwa na kauli mbiu isemayo; “Chukua Hatua Sasa Mimi, Wewe na Jamii” inalenga kuwajengea uelewa wa pamoja wafugaji na wataalamu juu ya namna bora ya kuwakinga na maambukizi ya kichaa cha mbwa ili kuipata jamii bora na iliyosalama dhidi ya ugonjwa wa kichaa cha mbwa.
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa