Timu ya usimamizi wa Miradi kuanzia ngazi ya Shule na Halmashauri wametakiwa kusimamia kwa karibu miradi inayotekelezwa na kufanya tathimini kwa kila hatua ili kuepuka matumizi mabaya ya rasilimali na kuhakikisha miradi hiyo inakamlika kwa wakati na kwa ubora unaotakiwa.
Hayo yameelezwa Septemba 24, 2025 na Mkuu wa Divisheni ya Elimu ya Msingi Bi. Zakia Fandey wakati wa kikao cha kufanya tathimini ya awali ya utekelezaji wa Miradi ya Ujenzi na Miundo mbinu ya Elimu msingi kupitia program ya BOOST kilichofanyika katika ukumbi wa halmashauri ya Wilaya ya Kilosa.
Bi. Zakia amesema ili kufikia malengo waliojikiwekea ni lazima kuwepo na ushirikiana wa pamoja na ushirikishwaji wa wananchi kujitolea nguvu kazi ili kupunguza gharama na kukamilisha mradi.
Naye Mkuu wa Kitengo cha Usimamizi na Ununuzi Bi. Grace Nyabange amewasihi wasimamizi hao kufuata kanuni na miongozo iliyopo kupitia mfumo wa NEST uku akiwasisitiza kutunza nyaraka zote za malipo.
Aidha, Mratibu wa Miradi ya BOOST Wilaya Ndg. Nelson Kiliba amesema kupitia kikao hicho kinachowakutanisha Wataalam wa Halmashauri, Wakuu wa Shule, Walimu wakuu, Watendaji wa kata na Wenyeviti wa vijiji ambapo kitaisaidi kwa kiasi kikubwa kupeana maelekezo , kutatua changamoto kwa wakati lakini pia kupeana uzoefu wa pamoja.
Akizungumza kwa niaba ya walimu , Mkuu wa Shule ya Sekondari Magole Mwl. Finyilise S. Elias amesema amepokea maelezo yote yaliyotolewa na kuahidi kuyafanyia kazi kwa ufanisi kwa maendeleo ya wilaya ya Kilosa.
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa