Imeelezwa kuwa ardhi ni mali ya watanzania wote na ndio usalama na amani yetu lakini pia maana ya dhana ya ardhi ni kielelezo cha uhuru wetu lakini pia uhai wetu kwamba ardhi isiposimamiwa vizuri ni usaliti kwa taifa.
Hayo yamebainishwa na Katibu Mkuu CCM Bashiru Ally katika mkutano wake na wananchi wa kata ya Msowero na kata za jirani na kusema kuwa CCM haitamvumilia yoyote ambaye atafanya kazi ya ulanguzi wa ardhi na kulimbikiza ardhi ambayo hawezi kuitumia kwa mujibu wa masharti na kwamba hayo ni mapambano ya kudumu ya kulinda taifa na rasilimali zake.
Bashiru amesema kuwa usimamizi mbovu wa ardhi hautakiwi na kwamba ni marufuku kwa mtu yoyote kugeuza ardhi ya umma kuwa gulio na kwamba mtu anapopewa ardhi kuna masharti yake asipoyatimiza ardhi itarejeshwa kwa umma na msimamizi mkuu ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Akizungumzia upande wa mashamba yaliyofutwa na mheshimiwa Rais wa awamu ya tano Bashiru amesema lengo la kufuta mashamba ni kuwapa kipaumbele wananchi kwa kufuata taratibu na sheria pamoja na kuzingatia mahitaji mahususi ya watu maskini
Aidha amewaagiza viongozi wote wa CCM ngazi ya zote wilayani Kilosa na mkoa wa Morogoro kuweka mfumo mzuri wa mawasiliano hasa ya ardhi kwani ukiwa kiongozi lazima utende haki na hupaswi kutumia madaraka yako kutenda dhuluma.
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa