Wagombea Ubunge Kupitia vyama mbalimbali vya Siasa wameendelea kujitokeza katika ofisi ya Msimamizi wa uchaguzi wa Jimbo la Kilosa na Mikumi Ndg. Joseph Kapere kwa ajili ya kuchukua ya uteuzi nafasi ya ubunge.
Ambapo leo Agosti 21, 2025 wagombea ubunge wane (4) wamejitokeza akiwemo Ndg.Joseph Linus Mdede kutoka chama cha MAKINI Jimbo la Mikumi, Ndg. Omary Salum Mtupe kutoka chama cha NCCR Mageuzi jimbola Kilosa, Ndg. HassanThabiti Mbaruku kutoka chama ACT- WazalendoJimbo la Kilosa na Ndg. Slas Ramadhani Kassao kutoka chama cha Wananchi (CUF) Jimbo mla Mikumi wamechukua fomu za uteuzi hivyo kufanya idadi ya wagombea kuongezeka.
Zoezi la Utoaji Fomu za uteuzi litahitimishwa rasmi siku ya jumatano tarehe 27 Agosti, 2025
“KURA YAKO N HAKI YAKO JITOKEZE KUPIGA KURA “.
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa