Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya Kilosa limepitisha Makisio ya bajeti ya shilingi bilioni 66,639,931,140 kwaajili ya mwaka wa fedha 2024/2025.
Hayo yamejiri februari 22,2024 wakati wa Mkutano maalum wa baraza la Madiwani kwaajili ya kupitisha Rasimu na mpango wa bajeti ya Halmashauri kwa mwaka wa fedha 2024/2025 uliofanyika katika Ukumbi wa FDC Ilonga, ambapo Halmashauri imekadiria kukusanya fedha za mapato ya ndani kiasi cha shilingi bilioni 6,628, 600,000, fedha za ruzuku kutoka Serikali kuu kwaajili ya mishahara na matumizi mengineyo na shilingi bilioni 60,011,331,140.
Akizungumza katika Mkutano huo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa Mhe.Wilfred Sumari ameipongeza Menejimenti na watumishi wote kwa ujumla kwa kuandaa bajeti hiyo sambamba na kupokea mapendekezo mbalimbali yaliyotolewa kwenye kikao hicho cha bajeti kwa lengo la kufanya marekebisho.
Aidha Mhe. Sumari ameipongeza serikali ya awamu ya sita kwa juhudi kubwa katika kuipatia Halmashauri fedha kwa ajili ya utekelezaji wa Miradi ya maendeleo kupitia wahesimiwa wabunge wa Majimbo ya Mikumi na Kilosa husasan katika miradi ya ‘BOOST na SEQUIP’ambayo imeleta mabadiliko makubwa katika jamii kwa kurahisisha mazingira ya kusomea na kufundishia na kupunguza mrundikano wa wanafunzi madarasani, pia kuepusha wanafunzi kutembea umbali mrefu kufuata shule jambo linalopelekea wanafunzi wengi kuwa watoro na pia kuharibikiwa.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi ambaye pia ni Mkuu wa Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu Ndg. Betuely J amesema kuwa amepokea mapendekezo yaliyotolewa katika mkutano huo na kusema kuwa kamati husika zitakaa kufanya marekebisho ya bajeti hiyo kwa kufanya maboresho kabla ya kuwasilisha katika kikao cha RCC.
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa