Wito umetolewa kwa watumishi wa halmashauri ya Wilaya ya Kilosa na wananchi wote ujumla kujenga utamaduni wa kufanya mazoezi ya mwili ili kujenga miili yao na kuifanya iwe imara wakati wote.
Wito huo umetolewa Oktoba 4, 2025 na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa Bi. Beatrice C. Mwinuka wakati akishiriki mazoezi ya pamoja na vikosi vya Ulinzi na Usalama Kilosa na Wadau mbalimbali katika Viwanja vya Shule ya Msingi Kilosa Town.
Bi. Beatrice amesema mazoezi ni muhimu kwa afya zao hivyo amewasihi watumishi hao kujitokeza kushiriki mazoezi hayo ya kila jumamosi kuanzia saa 12 asubuhi ili kuimarisha afya zao.
Kwa upande wake Mkuu wa Oparesheni Wilaya SP. Zabron Msusi amesema jeshi la polisi lipo tayari kuhakikisha hali ya ulinzi na usalama kwa raia na mali zao inakuwa shwari wakati wote.
Aidha amewataka wananchi kutoa ushirikiano wa kutosha kwa jeshi la polisi kwa kutoa taarifa za matukio ya vitendo viovu yanayotokea katika jamii zao kwa hatua zaidi za kisheria.
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa