Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa wamepatiwa mafunzo ya Kutumia mfumo wa manunuzi ya Umma NEST ili waweze kufanya manunuzi kwa urahisi na ufasaha kwa kufuata sheria ya manunuzi ya umma.
Mafunzo hayo yamefanyika Oktob 9, 2025 katika ukumbi wa Halmashauri yakiongozwa na Timu ya Mamlaka ya usimamizi na udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA) Kanda ya Pwani.
Mkufunzi wa Mafunzo hayo Dkt. Faustine Panga amesema Mfumo huo upo kwa ajiliya kusaidia Nchi lakini pia kuwawezesha watumishi kuufahamu na kuzingatia sheria za manunuzi kwa asilimia 100 hivyo kupunguza kero na malalamiko ya manunuzi.
Naye Mkuu wa Kitengo cha Usimamizi na Ununuzi Bi. Grace Nyabange ameishukuru Timu hiyo kwa mafunzo hayo na kuahidi kusimamia na kutekeleza yale yote waliyoelekeza.
Akizungumza kwa niaba ya watumishi wote Kaimi Mkuu Kitengo cha Usimamizi wa Taka Ngumu na Usafi wa Mazingira Ndg. Antony Mbise ameipongeza Timu ya PPRA kwa kuwajengea uwezo pia amepongeza Kitengo cha Usimamizi na Ununuzi kwa juhudi ya kuwasimamia kufanya manunuzi kwa kutumia mfumo huo wa NEST ambapo wamekuwa wakifanya vizuri ukilinganisha na Halmashauri zingine Mkoani Morogoro.
Mafunzo hayo yataendelea kwa muda wa siku tatu kwa watumishi wa makao makuu, watumiaji wa mfumo kutoka katika kila kituo cha kutolea huduma (lowel level) na Wazabuni wote wanaotoa huduma katika halmashauri ya Wilaya ya Kilosa.
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa