Serikali imepanga kujenga barabara yenye urefu wa zaidi ya kilometa 25 kwa kiwango cha Lami kutoka Miyombo hadi Kijiji cha Mbamba kilichopo kata ya Kilangali wilayani Kilosa ili kurahisisha shughuli za utalii katika Hifadhi ya Taifa ya Mikumi.
Kauli hiyo imetolewa 15 Agosti 2024, na Mkuu wa wilaya ya Kilosa Mhe. Shaka Hamdu Shaka wakati akiongea na wanachi wa kijiji cha Mbamba.
Mhe. Shaka amesema kuwa utekelezaji wa Mradi huo ni sehemu ya utekelezaji wa ahadi za Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan aliyoito wakati wa ziara yake ya kikazi hapa wilayani Kilosa lengo likiwa ni kuwarahisishia wanachi pamoja na watalii wanaosafiri na Treni ya Kisasa (SGR) kuelekea Hifadhi ya Taifa ya Mikumi.
Aidha Mhe. Shaka amewataka wananchi kutoa ushirikiano kwa wakandarasi wakati wa utekelezaji wa mradi huo ili ukamilike kwa wakati
Naye Diwani wa kata ya Kilangari Mhe. Amosi Thomasi ameishukuru serikali ya awamu ya sita kwa kuamua kuwajengea barabara kwa kiwango cha lami kwani barabara hiyo itachochea ukuaji wa uchumi wa wananchi wa kata ya Kilangali.
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa