Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Kilosa,Mhe Wilfred Sumari amewataka Watendaji wa Halmashauri kubuni vyanzo vipya vya mapato nje ya Kilimo ili kuepukana na kushuka kwa mapato pindi mabadiliko ya hali ya hewa yanapotokea na kuathiri sula la ukusanyaji wa mapato.
Mhe Sumari amesema hayo wakati wa Mkutano wa kawaida wa Baraza la Madiwani kwa kipindi cha robo ya pili (Oktoba –Disemba)2023/24 kilichofanyika katika ukumbi wa chuo cha FDC Ilonga Februari 21mwaka huu na kusema kuwa mabadiriko ya hali ya hewa kwa msimu huu yamesababisha uwepo wa mvua nyingi na mafuriko katika maeneo mengi Wilayani hapa na kupelekea mazao kuharibiwa jambo ambalo litasababisha ukusanyaji wa mapato kushukuka kwa namna moja ama nyingine.
Amesema ni muda muafaka kwa watendaji kubuni vyanzo vipya na vya uhakika nje na Kilimo ili kuboresha makusanyo ya Halmashauri na kuweza kuziba mapengo yanayoweza kutokea endapo kilimo kinapo sua sua kutokana na changamoto mbalimbali zinzosababishwa na mabadiriko ya hali ya hewa ikiwemo mafuriko,ukame na kadhalika.
Amesema kuwa sekta ya kilimo huchangia asilimia kubwa katika mapato ya Halmashauri hivyo kutokana na mvua zilizonyesha kwenye kipindi cha Disemba yameathiri shughuli za kilimo ambapo mazao yanatarajiwa kuwa machache hivyo kuathiri ukusanyaji wa mapato yatokanayo na kilimo,Katika hatua nyingine, wananchi wamesisitizwa suala la utunzaji wa mazingira ikiwemo vyanzo vya maji.
Akizungumza katika mkutano huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa Ndg. Michael Gwimile amewataka wananchi kutunza vyanzo vya maji ikiwemo kutokufanya shughuli ndani ya mita sitini kutoka kwenye vyanzo vya maji pamoja na kufuata maelekezo ya wataalamu.
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa