Baraza la bajeti limepitisha Mapendekezo ya Rasimu ya makisio ya mpango na bajeti ya Halmashauri ya wilaya ya Kilosa kwa mwaka wa fedha 2025/2026 ambapo amewapongeza Wataalamu wa Halmashauri kwa kazi nzuri ya kuandaa Mpango wa huo.
Akizungumza katika Mkutano huo wa Baraza la Madiwani kilichofanyika 25 februari 2025,katika ukumbi wa MT kwa ajili ya kupitisha Rasimu na mapendekezo ya mpango na bajeti ya Halmashauri kwa mwaka wa fedha 2025/2026, Mhe.Sumari amesema kwa mwaka wa fedha 2025/2026 halmashauri imekisia kukusanya na kutumia kiasi cha shilingi Bilioni sitini na nane milioni mia nne arobaini na tisa laki nne tisini na nane na kumi (68,449,498,010.83).
Amesema fedha hizo zinatarajiwa kukusanywa kutoka mapato ya ndani ya Halmashauri, Ruzuku ya serikali kuu na fedha kutoka kwa wahisani.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya kilosa Bi. Beatrice C. Mwinuka amesema kwa upande wa serikali kuu Halmashauri inatarajia kupokea kiasi cha shilingi 55,843,342,010.83, fedha kutoka kwa hisani shilingi 5,324,156,000 huku halmashauri ikitarajia kukusanya na kutumia kiasi cha shilingi shilingi 7,291,000,000 fedha kutoka katika mapato ya ndani ambapo kati ya hizo shilingi 5,602,275, 272.00 ni mapato halisi na shilingi 1,688,724,728 ni Mapato lidwa.
Pia Bi.Mwinuka amesema kuwa kutokana na mapato halisi ambayo ni shilingi 5,602,275,272.00 Halmashauri imetenga jumla ya kiasi cha shilingi 2,240,910,108.80 kwa ajili ya shughuli za maendeleo na shilingi 3,361,365,163.20 kwa ajili ya matumizi mengineyo .
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa