Hii ni mara baada ya kukamilika kwa Kiwanda cha kuchakata asali na kufanyiwa majaribio.
Hayo yamesemwa na Afisa Ufugaji Nyuki Bi. Diana Mahimbahi wakati wa zoezi la majaribio ya mitambo ya Kiwanda hicho Septemba 20, 2025.
"Kiwanda hiki kina uwezo wa kuchakata zaidi ya lita 3000 za asali za nyuki kwa siku " alisema Diana.
Pia ameongezea kuwa Kiwanda hicho kitatoa fursa kwa wanakijiji wa Maguha na vijini jirani kujipatia kipato kwa kuuza asali yao na kuwainua kiuchumi.
Akizungumza mara baada ya zoezi hilo , Bw. Jackson Martini (Mfugaji Nyuki) amesema kuwa walikuwa wanapata changamoto ya uchujaji wa asali lakini kwa sasa wanashukuru kwa kupata mashine hiyo ambayo inatumia muda mfupi kuchuja asali.
Naye Bi. Ludia Aron Mfugaji Nyuki amesema kuwa yeye pamoja na wafugaji wengine watanufaika na mradi huo kwa kuongeza kipato na biashara zao zitaimarika hivyo wamewashukuru MJUMITA kwa kuwapatia ofisi na mashine ya kuchuja asali.
Mradi huo wa uchakataji wa mazao ya Nyuki unatekelezwa na Mtandao wa Jamii wa Usimamizi wa Misitu Tanzania ( MJUMITA ) na kufadhiliwa na Shirika la Chakula Duniani (FAO) kupitia mradi wa Forest and Farm Facility (FFF).
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa