Serikali kwa kushirikiana na uongozi wa Wilaya ya Kilosa inatambua umuhimu na uwepo wa wazee pamoja na mchango wao katika jamii hususani katika kuleta chachu ya maendeleo sambamba na kuwahudumia wazee katika kutatua changamoto wanazopitia.
Hayo yamebainishwa na Katibu Tawala Wilaya Yohana Kasitila kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya wakati wa ufunguzi wa kikao cha viongozi wa baraza la wazee ambapo amesema kuwa Wilaya na Serikali kiujumla inatambua mchango wao huku akiwataka kuzingatia mwongozo ili ajenda zinazowahusu ziweze kuwekewa utaratibu na kuingizwa kwenye mpango wa Serikali na Halmashauri kwa ajili ya utekelezaji na kwamba Halmashauri ina wajibu wa kusimamia vizuri mwongozo huku akitaka changamoto na kero zote kuzungumzwa katika kikao kwa lengo la kupata utatuzi.
Pamoja na hayo amewaasa Maafisa Ustawi wa Jamii kutokwepa majukumu yao kwani mwongozo unawataka kuwa karibu na wazee ambao wana mchango mkubwa katika shughuli za maendeleo huku akisema kuwa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya itahakikisha mwongozo unafuatwa kikamilifu huku akisisitiza uwepo wa ushirikiano kutoka kwa wazee kwa kila hatua na pindi wanapohitajika wasisite kushirikiana na Wilaya sambamba na kushiriki na kuwa vinara katika kuhamasisha na kutoa elimu kwa wananchi kushiriki katika zoezi la Sensa ya Watu na Makazi inayotarajiwa kufanyika mwezi Agosti 2022.
Kwa upande wa viongozi baraza hilo wameupongeza uongozi wa Wilaya kwa kuwa karibu nao huku wakiiomba Halmashauri kuwapatia mradi wa bajaji ambayo wanaamini itakawasaidia kujikwamua kiuchumi jambo litakalowasaidia kuendesha shughuli zao pamoja na ofisi kwa ajili ya shughuli zao lakini pia wameiomba Idara ya Maendeleo ya Jamii hususani sehemu ya Ustawi wa Jamii kuwathamini na kuwajali.
Aidha wameomba kupewa kipaumbele katika mipango ya Halmashauri na upangaji wa bajeti kwa kutengewa fedha ambazo zitakuwa zikitumika katika kuendesha shughuli zao ikiwemo uendeshaji wa vikao na shughuli mbalimbali zinazohusu masuala ya wazee.
Mwenyekiti wa Baraza la Wazee Wilaya Leah Nzali
Afisa Ustawi wa Jamii Prisca Nivaco
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa