Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa kupitia Idara ya Maendeleo ya Jamii kwa kushirikiana na Chuo cha Maendeleo ya Wananchi (FDC) imeadhimisha Siku ya Familia Duniani kwa kufanya Bonanza la Michezo mbalimbali.
Bonanza hilo limefanyika leo, katika chuo cha Mendeleo ya Wananchi FDC Ilonga ambapo wanafunzi wa chuo hicho walipata fursa ya kushiriki michezo mbalimbali kama vile mchezo wa kuvuta kamba, kukuna nazi, kukimbia ukiwa umevaa kiroba, kukimbia ukiwa umefunika macho,kutembea na kijiko mdomoni pamoja na mashindano ya kunywa soda ambapo washindi walitangazwa na kupatiwa zawadi.
Akizungumza katika Bonanza hilo Kaimu Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi (FDC) Bw. Edwin Butaga amesema anaishukuru Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa kwa kuwafanya wawe sehemu ya ushiriki katika kuhitimisha maadhimisho hayo kwa kuwaletea bonanza la michezo chuoni hapo ambapo ni sehemu ya kuchangamsha mwili kiafya na kuwaunganisha pamoja. Pia wamejifunza mambo mbalimbali kupitia kongamano la vijana ambao walipatiwa elimu juu ya ustawi wa jamii katika kuboresha na kuimarisha wa familia bora.
Siku ya Familia Duniani Uazimishwa kila Mwaka 15, Mei ambapo kauli mbiu ya Mwaka huu inasema “Tukubali Tofauti Zetu kwenye Familia Kuimarisha Malezi ya Watoto.”
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa