Pongezi za dhati zimetolewa kwa serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na raisi wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kuipatia wilaya ya kilosa fedha kwa ajili ya utekelezaji wa mradi mbalimbali ya maendeleo.
Pongezi hizo zimetolowa katika Taarifa ya Mkuu wa wilaya ya Kilosa Mhe. Shaka Hamdu Shaka ya utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambayo ilisomwa na Mkuu wa Divisheni ya Elimu ya Sekondari Ndg. Joseph Kapere kwa niaba ya Mkuu wa wilaya katika Mkutano Mkuu wa Wajumbe wa Halmashauri ya Chama cha Mapinduzi ambao pia wakuu wa Idara na Vitengo wa Halmashauri ya wilaya na Taasisi walishiriki mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa Mamboya Februari 23, 2024.
Akisoma taarifa hiyo, amesema kuwa kwa kipindi cha Julai hadi Disemba 2023Wilaya imekuwa ikitekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo katika sekta ya huduma za kijamii na kiuchumi ambapo katika shughuli hizo, jumla ya shilingi 31,816,595,748.90 zilitumika kutekeleza miradi hiyo ndani ya Halmashauri ya wilaya ya Kilosa.
Aidha katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo imeelezwa kuwa kulitokea changamoto mbalimbali ikiwemo kuchelewa kwa matumizi ya fedha kutokana na changamoto za kimfumo, kupanda kwa gharama za vifaa vya ujenzi ikilinganishwa na kiasi cha fedha kinacholetwa pamoja na mafuriko yaliyoikumba wilaya ya Kilosa zimesababisha miradi kutokamilika kwa wakati.
Akiwasilisha taarifa ya Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA), Kaimu Meneja wa TARURA wilaya ya Kilosa Mhandisi Winston Mnyaga Amesema kuwa miradi kumi inaendelea kutekelezwa zikiwemo barabara, madaraja na makaravati huku miradi mingine ikitarajiwa kuanza ikiwemo ongezeko la Kilometa moja katika barabara ya Kidodi Vidunda itakayogharimu shilingi milioni 700,000,000.
Aidha ameipongeza serikali Pamoja na wabunge wa majimbo yote mawili kwa jitihada zao za kupambana kupata fedha za kutekeleza miradi ya maendeleo.
Imeelezwa kuwa halmashauri ya wilaya ya kilosa imeweka mikakati ili kukabiliana na changamoto hizo ikiwemo kuunda kikosi kazi ili kufanya ufuatiliaji wa miradi mara kwa mara na kuweka msukumo ili miradi yote iweze kukamilika kwa wakati.
Akitoa salamu za chama cha mapinduzi (CCM), Mwenyekiti wa chama hicho Ameri Mbaraka amewataka wakuu wa Idara na Vitengo kuhakikisha wanashirikiana na chama hicho katika kuitekeleza miradi kwani Raisi Samia anatoa fedha nyingi kwaajili ya miradi hiyo ya maendeleo wilayani humo.
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa