Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila amewataka wakulima kuzalisha mazao yenye viwango ili yaweze kuingia kwenye soko la ushindani wa kibiashara la kitaifa na kimataifa na kupelekea kuinua uchumi wa mkulima mmoja mmoja.
Hayo yamesemwa Julai 19, 2024 katika kikao cha kamati kuu ya maandalizi ya Nanenane kilichofanyika katika ukumbi wa Jeshi la Kujenga Taifa (J.K.T) nanenane ambapo Mhe. Chalamila amesema maonesho ya nanenane ya mwaka huu kutakuwa na mazao yatakayoweza kuingia kwenye ushindani wenye tija.
Pia Mhe.Chalamila ambaye pia ni Mwenyekiti wa kamati kuu ya maandalizi ya nanenane amewataka wakulima, wafugaji na wavuvi kujitokeza kwa wingi kushiriki maonesho hayo ambayo ni fursa kwao kujifunza na kujionea teknolojia mbalimbali za kilimo.
“waje kwa wingi ili waweze kuona vipando,mazao, mifugo na kuona teknolojia nyingine nyingi za kilimo ambazo leo tupo kwenye kilimo kinacholenga zaidi kudhibiti kasi ya mabadiliko ya tabia nchi.” amesema Mhe. Chalamila.
Aidha Mhe. Chalamila ameishukuru serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.dkt. Samia Suluhu Hassani kwa kuendelea kutenga fedha kwa ajili ya kuboresha sekta ya kilimo kutoka kilimo siasa kwenda kwenye kilimo uchumi.
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa