Imebainika kuwa mchango wa mwanachama kwa ajili ya mfuko wa afya ya jamii CHF iliyoboreshwa gharama zake zimebadilika kutoka shilingi 10,000 hadi 30,000 kwa kaya kwa mwaka ikiwa ni mwongozo uliotolewa katika waraka namba moja wa maboresho ya mfuko wa afya ya jamii CHF ambao umeanza kutumika rasmi hapa nchini kuanzia tarehe 01/05/2018.
Hayo yamebainishwa Julai 12, 2018 na Mratibu wa CHF iliyoboreshwa Wilaya ya Kilosa Maxmillan Ndwangira katika mafunzo ya siku mbili kwa maafisa waandikishaji wa CHF iliyoboreshwa ambapo amesema kuwa mabadiliko hayo wilayani Kilosa yanatarajiwa kuanza tarehe 14/07/2018.
Ndwangira amesema kuwa kwasasa mafunzo hayo yanatolewa kwa maafisa waandikishaji kwa ngazi ya vijiji ambapo mafunzo hayo yanalenga kuihamasisha jamii kujiunga na mfuko huo lakini pia kujifunza matumizi ya mfumo mpya wa uandikishaji katika simu ujulikanao kama Insurance Management Information System(IMIS)
Aidha niseme kuwa matibabu kupitia kadi ya CHF iliyoboreshwa yatakuwa yakipatikana kuanzia ngazi ya zahanati, kituo cha afya, hospitali ya wilaya na hospitali ya mkoa kwa mfumo wa rufaa
Naye mwezeshaji wa mafunzo hayo James Kidumba kutoka mradi wa HPSS amesema lengo la waraka huo ni kuleta tija na ufanisi katika uratibu na utoaji huduma ya mfuko wa jamii ili kufikia malengo ya kitaifa na kwamba wananchi ambao wameshalipia mchango huo lakini bado hawajapokea kadi zao watapatiwa kadi hizo kwa gharama ile waliyolipia awali.
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa