Timu ya Menejimenti ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa imefanya ziara ya kutembelea na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo yenye thamani ya shilingi Bilioni 4.4 inyotekelezwa wilayani hapo iliyolenga kuhakikisha miradi yote inatekelezwa kwa wakati na kwa ubora unaotakiwa.
Ziara hiyo ya siku mbili imefanyika Agosti 18-19, 2025 ikiongozwa na Mwenyekiti wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa Bi. Beatrice C. Mwinuka ambapo timu hiyo imetembelea mbalimbali ikwemo Ujenzi wa Soko la Ruaha,Ujenzi wa Shule mpya ya Sekondari ikiwemo Kifinga, Mamba, Uponela pamoja na Ujenzi wa shule za Msingi ambazo ni Uponela na Nyali.
Akiwa katika eneo la Mradi wa ujenzi wa Soko la Ruaha Bi. Beatrice ameagiza taratibu za ujenzi wa soko hilo zianze kufanyiwa kazi haraka iwezekanavyo ili ujenzi huo uweze kuanza kabla ya mwezi Agosti kuisha.
Pia Bi. Beatrice amemtaka Afisa Ardhi kukamilisha taratibu za upatikanaji wa hati miliki ili kuepuka uvamizi wa ardhi katika eneo la mradi huku akisisitiza shughuli za ujenzi ziweze kuanza na kuongeza kuwa kwa miradi ambayo ipo hatua ya mwisho kumalizia kazi zilizobaki kabla ya msimu wa mvua kuanza.
Aidha, Mkurugenzi huyo amewata wasimamizi wa Miradi kuanzia ngazi ya kjiji, Kata na Wilaya kuendelea kushirikiana kwa karibu ili kutatua changamoto zinazojitokeza wakati wa utekelezaji wa mradi lengo likiwa ni kuhakikisha miradi yote inakamilika kwa wakati ukiokusudiwa .
Nao Wajumbe wa CMT wameshauri kuwepo na uwazi wa taarifa za miradi bila kificho n ili kuepuka malalamiko katika kamati zinazosimamia ujenzi wa miradi hiyo ya maendeleo pamoja na ushirikishwaji wa nguvu za wananchi.
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa