Timu ya Menejimenti ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa (CMT) ikiongozwa na mwenyekiti wake Daud Mchilu imefanya ziara ya kutembelea na kukagua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.
Akizungumza wakati wa ziara hiyo iliyofanyika 20 Februari, 2025 Mchilu amewataka viongozi wa shule zinazosimamia miradi kwa kushirikiana na viongozi wa vijiji kuchukua hatua na kutatua changamoto zinazojitokeza katika eneo la mradi lakini pia kutoa taarifa kwa changamoto zilizokosa utatuzi kwa idara husika ambapo zitatatuliwa kwa haraka ili miradi hiyo iweze kukamilika kwa wakati uliokusudiwa.
Sambamba na hayo Wajumbe hao wa CMT wametoa ushauri kwa wasimamizi wa miradi kuzingatia na kutunza nyaraka za miradi kuanzia hatua ya mwanzo hadi hatua ya mwisho ya ujenzi.
Miradi iliyotembelewa na timu hiyo ni pamoja na ujenzi wa shule ya sekondari Chanzuru, Madoto, Ujenzi wa shule mpya ya msingi Matongolo,ujenzi wa shule mpya ya sekondari Amali, Mwandi na nyumba za walimu ambapo miradi hiyo itasaidia kupunguza msongamano wa wanafunzi katika shule mama, kuondoa adha ya wanafunzi kutembea umbali mrefu, utoro shuleni lakini pia kutoa elimu bora.
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa