Imeelezwa kuwa Daraja la Dumila,Wilayani Kilosa halitahamishwa kama ilivyopangwa hapo awali na badala yake litaimarishwa ili liweze kuwa imara zaidi na kuendelelea kutumika .
Hayo yameelezwa february 22,2024 na Waziri na Waziri mwenye dhamana Mhe.Innocent Bashungwa wakati wa ziara yake Wilayani Kilosa ya kukagua Daraja la Dumila ambalo mara kadhaa limekuwa tishio kwa wasafiri wa Barabara ya Dar es Salaam – Dodoma na Mikoa ya Kaskazini kutokana na Daraji hilo kujaa mchanga.
Mhe Bashungwa amesema kuwa ili kutatua changamoto hiyo Serikali kupitia Wataalam wa Wizara ya ujenzi walifikia uamuzi wa kuchepusha Barabara hiyo kupita eneo la juu la mto huo kilomita 10 kutoka Daraja lilipo sasa na kujenga Daraja lingine,hata hivyo Waziri ameagiza Watendaji wake kutochepusha Barabara hiyo na Daraja hilo kubaki mahali lilipo na badala yake walihimarishe zaidi kwa kuwa tayari kuna uwekezaji mkubwa wa watu na Serikali katika mji wa Dumila.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe Adam Kighoma Malima ameendelea kuwaomba radhi watu wa Dumila kutokana na kadhia ya maji yanayotokana na mto kuacha njia yake hivyo kumwaga maji katika makazi ya watu na kuwahakikishia kuwa Serikali ya awamu ya sita iko mbioni kushughulikia kadhia hiyo.
Aidha ameendelea kumwomba Waziri wa ujenzi kwa kushirikiana na Wizara ya Kilimo kuona uwezekano wa kujenga mabwawa juu ya mto huo ili kupunguza kasi ya maji hayo na kutumika katika shughuli za kilimo na shughuli nyingine za kibinadamu
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa